#HEKIMA YA LEO: Kama Hufurahi Wewe Huishi.

Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Maisha ni kufurahi, haina maana kwamba utakuwa unapitia mambo ya kukufanya ufurahi kila siku lakini unatakiwa kufurahi.

Kuna msemo umezoeleka sana unasema “cheka uongeze siku za kuishi” ni kweli kama hucheki unazeesha seli za mwili wako.

Unapokosa furaha hata utendaji wako wa kazi unakuwa mbovu.
Utendaji kazi wa baadhi ya viungo vya mwili unakuwa mbovu.
Kuna baadhi ya magonjwa yataanza kuibuka kwasababu tu huna furaha.

Nikutie moyo pamoja na hali ngumu ya maisha unayopitia tafuta jambo moja litakaloweza kukufurahisha kila siku na uwe unalifanya. Jambo hili liwe ni jambo chanya.

Una sababu ya kuwa na furaha,
Sababu ya kwanza ni uhai wa bure ulionao.
Sababu ya pili ni nguvu ulizonazo.
Sababu ya tatu ni watu tunaokupenda kama sisi na tunakuandikia kila siku ili tu uweze kusonga mbele.

Usiache kufurahi maisha ni mafupi sana kwa mtu ambaye ananuna kila saa na anakwazika kila saa.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

This entry was posted in USIISHIE NJIANI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *