#HEKIMA YA LEO: Kanuni ya J+F Inavyoleta Matokeo.

jacobmushi
2 Min Read

Habari Rafiki, siku yako umeianzaje? Unajua kwamba jinsi unavyoanza siku yako ndio na matokeo hufanana hivyo hivyo? Kama umeanza kwa kulalamika basi siku nzima inakuwa ni kulalamika. Chagua kuanza siku yako vizuri ili uwe na matokeo bora.

Amka Mapema,

Sali,

Soma Kitabu,

Pangilia Siku yako.

Fanya Mazoezi.

Leo nakuletea kanuni ya J+F yaani Jua kisha Fanya. Tunajifunza kila siku lakini unaweza kukuta wewe huna mabadiliko yeyote na mwenzako upo nae hapa hapa anajifunza haya haya lakini anaona mabadiliko. Unachotakiwa kufanya hapa ni kuchukua Hatua mara moja kwa kila ambalo unajifunza.

Ukiwa mtu wa kuahirisha yale ambayo unajifunza na kusema utafanyia kazi kesho au keshokutwa utajikuta ni mtu ambaye unajaza vitu vingi hadi unavisahau. Chochote unachojifunza fanyia kazi mara moja kwa kadiri inavyowezekana.

Kanuni hii ndio inakupa mwangaza wa kule unapoelekea. Umejifunza kwa kupitia Makala andika kwenye notebook yako yale ya kufanyia kazi na uyaweke kwenye vitendo mara moja. Baada ya muda utaona mabadiliko ya haraka kwenye Maisha yako.

Kinyume na hapo utaendelea kusema Makala hii nzuri sana, nimejifunza kitu hapa. Kweli msiache kuendelea kutuma vitu vizuri, lakini hakuna kinachobadilika.

Jua, Fanya. Umepata maarifa mapya chukua Hatua usisubiri uone matokeo kwa wengine fanya watu waje wajifunze kwako. Fanya watu waje wakutolee mfano wewe.

Usiache kuwashirikisha wengine Makala hii.

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading