#HEKIMA YA LEO: Kimbizana Na Ndoto Zako.

jacobmushi
1 Min Read

Hello, Unatumia Mtandao wa Instagram?

Bonyeza hapa uni follow ili upate madini ninayoweka kila siku… http://www.instagram.com/jacobmushi

Wakati wengine wanakimbizana na fasheni mpya wewe Kimbizana na ndoto yako.

Wakati kila mmoja anataka kujionyesha kwa watu, wewe onyesha ndoto zako.

Wakati wengine wanakimbizana na matukio wewe Kimbizana na bidhaa zako.

Acha kufuata mkumbo, maisha yako sio ya maonyesho, fanya vitu watu wataanza kukutolea mfano wenyewe.

Ndoto Yako ni ya muhimu sana katika Maisha yako. Haya mengine yavumilie tu.

Watu wamekuwa ni wafuataji wa kila kinachoendelea kuliko hata mambo ya muhimu kwenye maisha yao.

Wewe ni nani anaefuatilia maisha yako?
Kuna nini unafanya kitaleta matokeo makubwa miaka ijayo?

Anza Sasa, Ndoto Yako Inawezekana.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading