#HEKIMA YA LEO: Kipimo Cha Ukomavu.

By | March 29, 2018

Kipimo cha Ukomavu wako kinatokea pale ambapo unatakiwa uwatendee mema watu ambao hawastahili kabisa katika akili za kibinadamu. 

Watu wengi hushindwa mtihani huu.

Kuwa mwema hata kwa Waliokuumiza sana.
Waliokusaliti kwenye mambo makubwa.
Wabaya wako ambao ulisema hutakaa uwasamehe kabisa.

Hawa watu mara nyingi wanapokuja kwetu kutuomba msaada tunaweza kuwatendea ubaya kama malipo. Lakini kwa Mungu Kipimo cha wewe kukomaa na kukua ni kuweza kuwatendea mema watu wa aina hii.

Wengi hapa tunakwama sana, wabaya wetu wanapopatwa na matatizo tunafurahia na kuona ni Mungu amewadhibu. Kumbe wakati mwingine ni Kipimo kwako wewe.

Ni bora usikie kwa watu fulani aliekufanyia mabaya amepatwa na shida, lakini inapotokea wewe unamuona akipitia magumu unapaswa kutenda wema bila ya kujali alichokufanyia.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *