Unajua mboga tamu ilipitia maumivu kwenye moto mkali jikoni. Ni rahisi sana kusifia utamu wa mboga bila ya kujua ni gharama gani imelipwa wakati wa kuitengeneza. Ili mboga iwe tamu lazima kuwa na mchanganyiko wa viungo ambavyo vitaleta ladha ya tofauti.

Ladha ya mboga inatokana na mchanganyiko wa viungo. Kwenye Maisha ili uweze kuwa wa tofauti inategemea na yale mambo ambayo unapitia kila siku. Kama utaishi aina ya Maisha yenye hali moja inayofanana tu Maisha yako yanaweza kukosa ladha nzuri.

Lazima ukubali kupitia mchanganyiko wa watu tofauti tofauti na tabia zao. Kwa kupitia mchanganyiko huo ndio unatengenezwa na kuwa mtu bora. Kila mtu ambaye unakutana nae ni sawa na kiungo ambacho kimechanganywa kwenye mboga.

Kubali kutengenezwa, kubali kuumia ili uje kuwa na ladha ya tofauti kwenye Maisha yako. Kila mwenye Maisha ambayo unayatamani alipitia kutengenezwa hadi akaiva. Wewe usipokubali kutengenezwa utakuwa sawa na mboga iliyopikwa bila ya viungo. Ladha haiwezi kufanana na mboga yenye viungo mbalimbali.

Maisha yako yatawavutia watu kuja kujifunza kutokana na namna ulivyoyaishi. Kama vile ilivyo harufu ya mboga unavyowatamanisha majirani. Kama usipokubali kupambana na kujifunza kwenye kila hali, ukawa mtu wa kukata tamaa na kurudi nyuma utakuwa sawa na mboga isiyo na ladha wa harufu. Hakuna anaeitamani kwasababu hakuna anaejua kama ipo.

Maisha yako ni mchanganyiko wa hali na tabia za watu ambao umekutana nao na ukajifunza kwao. Wapo ambao wamekuumiza, lakini ulitoka na somo , wapo waliokufanya ukafurahi pia ulitoka na somo.

Hakikisha unakubali kutengenezwa kwa kila hali inayokuja kwenye Maisha yako.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading