Connect with us

#HEKIMA YA LEO: Kuwa Sehemu Ya Tukio.

USIISHIE NJIANI

#HEKIMA YA LEO: Kuwa Sehemu Ya Tukio.

Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi. Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote. “NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA. MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.” Kuna msemo usisubiri embe chini ya mnazi. Yaani kile unachokitaka siku […]

Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Kuna msemo usisubiri embe chini ya mnazi. Yaani kile unachokitaka siku zote kinapatikana kule kinapotakiwa kuwepo.

Ukikaa nyumbani halafu unasema maisha ya magumu ni wewe umeamua mwenyewe.

Ukikaa na wapumbavu halafu ukategemea uwe na maarifa utakuwa unajidanganya.

Penda kujihusisha na kule kunapoleta matokeo ya maisha yako.

Tunda siku zote halianguki mbali na mti wake, yale yanayowatoka watu ndio yamewajaa.

Kuna mtu anasema hali ni ngumu lakini muda wake mwingi kauweka kwenye kufuatilia maisha ya wengine.

Kuwa sehemu ambayo unatakiwa kuwepo lazima utaziona fursa.
Ukikaa sehemu za watu utaishia kulalamika siku zote.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

Continue Reading
You may also like...

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in USIISHIE NJIANI

To Top