#HEKIMA YA LEO: Njia Rahisi Inaweza Kugeuka Kuwa Ngumu Sana.

Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Watu wengi hutafuta njia rahisi za kufanya mambo yao, sasa tatizo halipo kwenye njia rahisi. Swali la kujiuliza ni je hiyo njia inaleta suluhisho la kudumu kwenye tatizo!?

Mara nyingi njia rahisi zinaweza kuwa sababu ya mambo kufanyika chini ya kiwango. N wengi huzitafufa njia hizi ili kukwepa gharama fulani.

Sasa zile gharama ambazo zinakwepwa huja kuleta gharama kubwa zaidi mbeleni.

Kwenye safari ya mafanikio usipende sana kuangalia kirahisi ni kipi bali angalia sahihi ni kipi. Je kinaleta yale matokeo yanayotakiwa?

Penda kujiuliza maswali ili ujue matokeo ya hatua unazotaka kuchukua.

Usikubali kukwepa kulipa gharama maana utakuja kuilipa tu siku moja.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

This entry was posted in USIISHIE NJIANI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *