Bonyeza hapa upate offa ya Vitabu Bora Mwezi April. https://jacobmushi.com/offa-offa-offa-ya-vitabu-bora-mwezi-april/
Tafuta kawaida nyingine kabla hiyo uliyoipata hujaizoea. Mwanzoni unaweza kuona kuna ugumu wa kutimiza jambo Fulani lakini ukishalitimiza unaanza kugundua kumbe ilikuwa ni hivi. Mtoto anapoweza kutambaa hatakiwi kubakia kwenye kutambaa yaani akishazoea tu kutambaa basi anatakiwa aanze kujifunza kusimama na kisha kutembea na kukimbia kabisa. Wewe pia unapoweza kimoja basi jipe kazi nyingine mpya haraka ili uweze kupanda viwango Zaidi na Zaidi.
Kwenye Maisha kuna mambo ambayo unakuwa na hamasa kubwa sana kuyafanya na ukiweza kuyafanya baada ya muda unaanza kuona ni kawaida tu. Yaani ni sawa na mtu ambaye alikuwa anatamani sana kwenda kuishi sehemu Fulani mashuhuri sana baada ya kufika mwanzoni atakuwa na furaha sana, nguvu mpya lakini baada ya kupazoea anaanza kuona tena ni kwa kawaida.
Vile vile unapokuwa na malengo yako makubwa ukishayatimiza unakuwa na nguvu mpya, na furaha sana. Lakini ukipita muda kidogo unakuwa wa kawaida kama vile hakuna kilichotokea.
Unachopaswa kutambua ni kwamba Maisha ni kama safari ambayo haina mwisho. Kila siku kuna sehemu unatakiwa uvuke. Kuna sehemu utapanda mlima, sehemu nyingine ni bonde. Kila siku ni nafasi ya wewe kusonga mbele Zaidi.
Unapotimiza lengo moja usisubirie mpaka uone imekuwa kawaida kabisa ndipo uanze tena kutimiza lengo linguine. Nguvu ile uliyoipata kwa kufanikisha jambo moja itumie kufanikisha lengo linguine. Hamasa ile uliyoipata kwa kutimiza mpango mmoja itumie kufanikisha mpango mwingine.
Usikubali kusubiri hadi ile furaha na nguvu ulizopata zipotee ndipo uanze tena. Kama ni biashara jana uliweza kuuza sana basi usibakie na zile sifa za jana za kuuza sana bali utumie nguvu hiyo kuendelea kuuza Zaidi.
Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Songambele, Timiza Ndoto Yako.”
Nice one bro ?
Asante Sana Rafiki