Kila mmoja wetu kutokana na anachokifanya kuna mtu aliefanikiwa zaidi yake. Ni muhimu sana kujua unaemtazama na ni vitu gani unajifunza kwake.

Hakuna mtu ambaye atakuwa anaenda tu bila kuwa na mtu anaemwangalia.
Unapaswa kujifunza sana ujue ni mbinu gani wanatumia hadi wanapata matokeo makubwa.

Usikubali kubaki kama mtu asiye na mwelekeo wa maisha. Wapo watu unaweza kujifunza kwao.

Kitu cha muhimu unapaswa kujua ni kwamba usiwe unaiga, bali ujifunze. Ukikosea utakuwa nakala ya yule unaemtazama.

Unachotakiwa kujifunza ni mbinu za kufanikiwa, mbinu za kupata matokeo makubwa.

Kwa ulimwengu wa sasa unaweza kumtafuta mtu unaetaka kujifunza kwake kwa kupitia mtandao tu. Unaweza kujifunza mengi sana na ukajikuta unapiga hatua kila siku.

Usiache kupata offa yako hapa..

Offa Offa Offa, Ya Vitabu Bora Mwezi April.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading