#HEKIMA YA LEO: Unyenyekevu Utakulinda.

jacobmushi
1 Min Read

Unawafahamu watu ambao wakiwa na shida wanakuja kwako kwa upole wakinyenyekea sana. 

Lakini wakishapata wanasahau na kuanza kuonyesha tabia zao halisi.

Wako watu wa aina hii wengi kwenye jamii yetu. Wakiwa chini wanakuwa wanyenyekevu na wapole sana.

Wakipata fedha au cheo utaanza kujua tabia zao za kweli.

Rafiki yangu nakuomba usiwe mmoja watu wa aina hii. Ili uweze kudumu kwenye mafanikio kamwe usikubali kuacha unyenyekevu.

Unyenyekevu Utakulinda popote utakapokuwa.
Unyenyekevu utakukutanisha na watu wakubwa.
Unyenyekevu utakupa nafasi kubwa ambazo hukuwahi kutarajia.

Usikubali kuuacha huu ndio ulinzi wako. Pale tu utakapoanza kuonyesha tabia zako wale waliokuamini hawatakuamini tena.

Usisahau Ulipotoka.

Offa Offa Offa, Ya Vitabu Bora Mwezi April. https://jacobmushi.com/offa-offa-offa-ya-vitabu-bora-mwezi-april/

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading