Siku zote amri inapotolewa kinachofuata huwa ni Utii na unaposhindwa kutii amri maana yake wewe unakuwa muasi. Kwa serikali zetu ukiasi kinachokujia ni hukumu wakati mwingine hata kifo kutegemea na yule aliekupa amri.
Sasa tukisoma kwenye neno la Mungu Yohana. 13:34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Maana yake kupendana na ndugu zako, watu waliokuzunguka, ni amri sio ombi, sio kitu unabembelezwa ufanye; kinyume chake sasa ukichukia wewe unakuwa muasi unakuwa umeiasi amri hii ya upendo.
Huwezi kusema unampenda Mungu usiomwona wakati unamchukia ndugu yako ambaye unamwona.
Kwanini tunapaswa kuhimiza upendo?
Bila ya Upendo Hakuna Amani.
Bila ya Upendo hakuna furaha.
Bila ya Upendo Hakuna maendeleo.
Bila ya Upendo tutaishia Kuuana tu.
Kama humpendi mtu huwezi kufurahia mafanikio yake, huwezi kuhamasika na mafanikio yako, huwezi kujifunza kwa yule unaemchukia. Jifunze kupenda wengine ili uweze kujifunza kwao.
Yeye alitupenda akautoa uhai wake kwa ajili yetu na mpaka sasa kuna mabilioni ya watu wanamtumikia. Hivyo basi ili wewe uweze kupokea upendo kwa wengine hakikisha unatoa upendo. Hata kwa wale wanaokuchukia hakikisha unawaonesha upendo.
Soma: Kristo Angeondoka Bila Ya Kuzungumzia Kurudi mara Ya Pili Ingekuaje?
Hata wale waliokutendea ubaya wa kila namna waoneshe upendo. Kwa kufanya hivyo utajitengenezea njia bora ya mafanikio kwenye Maisha yako.
Tafakari sasa hivi ni mtu gani ambaye ukimfikiria unasikia uchungu? Kwanini unaendelea kuubeba uchungu ndani yako? Naomba leo umwambie nimekusamehe, nimekuachilia, halafu uendelee na Maisha yako.
Wapo wengi wamekutendea mambo mabaya sana hata hayafai kuelezea hadharani kwasababu yanaweza kukufanya uchafuke najua inauma sana, najua imekua doa kubwa sana. Embu jiulize yeye alieteswa uchi msalabani bila ya kosa lolote angekufa bila ya kusamehe ingekuaje? Wewe inakuaje unashindwa kusema Nimewasamehe Nawapenda sana wale walionitendea mabaya.
Upendo Pekee ndio Kisasi cha kweli.
Nakutakia Kila la Kheri
Rafiki yako
Jacob Mushi.
Mkuu sawa umenena vema. .kuna muda nilikuwa natafakari kipi kigumu katika kusamehe na kwa nini watu hatusamehe. nilichogundua ni kwamba kinachosababisha ni ule uchungu tunapokuwa nao .
Mtu akikikumbuka uchungu anaishia kusema sina namna ya kujirudishia kisasi na ku pretend kama kasemehe..
I wish siku moja ufundishe namna ya kuondoa uchungu kwa yule aliyekukuosea …Ubarikiwe
Amina Ubarikiwe sana, ukweli uchungu ndio kisababishi kikubwa kuzuia msamaha, na inahitaji uwezo wa hali ya juu kuondoa uchungu kwasababu unaweza kuachiwa alama ya Maisha, tuende pamoja nitaandaa somo