Ni vyema kuelewa kwamba kuna tofauti ya kuwa chanya kwenye mambo na kupotezea ukweli halisi wa jambo lenyewe.
Kuna nyakati ili uweze kutatua mambo kwenye maisha yako inakupasa uanze kuyaelewa hayo mambo yakoje.
Mfano una matatizo kwenye familia yako hata ukiwa chanya kivipi, na ukaweza kuyaona hayo matatizo sio kitu hakubadilishi ukweli kwamba hayo ni matatizo.
Kwa lugha rahisi tunaweza kusema hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo (Mwalimu Nyerere).
Kuna Wakati unaweza kuwa chanya kiasi kwamba ukawa unajidanganya kwamba hakuna matatizo.
Kuelewa matatizo uliyonayo sio kwamba wewe una mawazo hasi. Unayaelewa ili uweze kuyatatua, usipoyaelewa huwezi kujua ni jinsi gani utaweza kutatua.
Usikimbie Matatizo kwa kujidanganya yatakwisha kwa kubadili tu namna unavyofikiri. Lazima uje kwenye hatua ya kutafuta suluhisho.
Fikiri Chanya lakini usiishie kwenye kufikiri nenda hatua nyingine ya kutatua yale matatizo yako.
Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/