“It isn’t what you have or who you are or where you are or what you are doing that makes you happy or unhappy. It is what you think about it.”
― Dale Carnegie, How to Win Friends and Influence People

Mwandishi Dale Carnegie anasema katika kitabu chake kwamba, SIO KILE ULICHONACHO AU VILE ULIVYO AU PALE ULIPO AU KILE UNACHOKIFANYA NDIO KINAFANYA UWE NA FURAHA AU UKOSE FURAHA. NI KILE UNACHOFIKIRI.

Mtu amekusema kwa ubaya kusemwa hakukufanyi ukose furaha, maneno Mabaya hayakufanyi ukose furaha, bali fikra zako tu. Vile utakavyoanza kumfikiria yule mtu na yale maneno ndio vitafanya uwe na furaha au usiwe na furaha.

Ukiamua kumpuuza aliekusema vibaya utakuwa na amani na furaha. Ukiamua kuwaza ndani na Kusema hakupendi, anakuonea wivu na mengine mengi utaanza kukosa furaha na kukonda.

Furaha ni fikra, kile unachofikiria.

Unaweza kuamua kufurahia kazi unayofanya sasa au ukabaki unanung’unika kwasababu tu hupati kile unachokitaka.

Unaweza kuamua kufurahia mahusiano kwa kubadilisha fikra zako juu ya yale matendo unayoona unatendewa.

Kama mtu hakujali au hakufanyii vitu fulani wanavyofanyiwa wengine au ulivyowahi kufanyiwa na mwingine wewe acha kufikiria kwamba labda hakupendi. Badilisha mtazamo wako amua kufiri kwa namna itakayokuletea matokeo Chanya.

Kuwa na furaha au kutokuwa na furaha ni tafsiri unayojipa ya kile kinachoendelea kwenye Maisha yako.

Watu wawili wanaweza kupitia hali moja inayofanana mmoja akakata tamaa na mwingine akaendelea mbele na usijue kabisa kama alishapitia magumu.

Wewe unatafsiri vipi yale yanayooendelea kwenye Maisha yako? Kama umekuwa huna furaha kwenye jambo lolote jaribu kuangalia wewe ulikuwa unafikiri vipi halafu badilisha fikra zako juu ya jambo hilo.

Nakutakia Kila la Kheri.

Rafiki Yako

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading