Wakati tumebakiwa na siku tatu pekee tufikie mwaka mpya 2018 nimeona nikueleze juu ya dhambi hii mpya ambayo unatakiwa usiitende kabisa kwenye Maisha yako kuanzia mwaka 2018. Kwanza kabisa najua umeshaweka malengo yako na mambo mengine mengi lakini unapaswa kujua kwamba kama hutaweza kuweka bayana vitu ambavyo hutavifanya mwaka 2018 basi hivyo ulivyosema utakwenda kufanya havina nguvu sana.

Ili yale ambayo unasema utakwenda kufanya yapate nguvu ni vyema ukaweka chini na mambo ambayo hutayafanya kabisa mwaka 2018.
Dhambi hii mpya ni kukosa fedha mfukoni mwako. Kama kuna dhambi ambayo hupaswi kuitenda tena kuanzia mwakani ni kukosa fedha mfukoni mwako. Leo na kesho baada ya kusoma Makala hii naomba ukae utafakari ni kiwango gani cha pesa ambacho utatamani kiwe kinakuwepo mara zote kwenye mfuko wako wa fedha. Nikiwa na maanisha kwenye pochi yako.

Soma: Hapa Ndipo Unakosea Kuhusu jana Yako 

Fedha hizi sio za akiba, sio za mambo mengine yeyote kwenye Maisha ila ni pesa ambayo unabakia nayo baada ya kutoa hayo mengine ya muhimu. Ukiweza kuweka kiwango kizuri basi ina maana kwamba utafanya kazi kwa bidi ili upate pesa za kutoa kwenye mahitaji mengine na ubakiwe na pesa.
Jiwekee kiwango ambacho unajua kabisa hiki sijawahi kuwa nacho mara kwa mara na upambane hadi ufikie kwenye kiwango hicho. Kama mara nyingi umekuwa hukosi elfu kumi basi ongeza mara mbili au mara tatu yake.
Kumbuka hapa nazungumzia pesa inayobaki baada ya mambo yote ya muhimu kama matumizi, akiba, sadaka, uwekezaji, utoaji, na mengine yote ya muhimu.
Ni dhambi kubwa sana kwako wewe kukosa hicho kiwango ambacho umejiwekea. Endelea kuongeza bidii ili usiitende tena dhambi hii.
Mwaka 2018 ukawe mwaka wenye mabadiliko makubwa kwenye maisha yako

” Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   
Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading