Habari za leo rafiki. Naamini umeanza siku yako vyema kabisa ili kuongeza hatua kuifikia ndoto yako. Vile unavyoanza siku yako ndio itakavyokuwa. Ukianza kwa kukasirika siku yako itakuwa hivyo. Ukianza kwa ushindi na furaha tele siku yako itakuletea furaha na ushindi.
Moja ya tabia ambayo naipigia kelele kila wakati kwamba haifai kwenye maisha yetu ni tabia ya ubinafsi. Ubinafsi ninaouzungumzia mimi ni ule wa kutaka kupata pekee yako bila ya kutoa chochote. Shida ambayo utapata ukiwa na tabia ni kwamba utakuwa kama ombaomba kwasababu hauna unachotoa.
Siku moja nimekutana na rafiki yangu niliyesoma nae akaniambia yeye tayari ameshapata kazi yake nzuri na anapokea mshahara mzuri ambao unamwezesha kuyabeba mahitaji yake yote ya muhimu kwenye maisha yake. Kitu cha ajabu akanishangaa sana mimi kwanini hadi sasa sijaamua kutafuta kazi. Kwa biashara nilizokuwa nafanya akaniona kama mtu anayejisumbua sana.
Akasema sasa wewe unateseka kote huko ya nini si utafute kazi unakaa tu unalipwa mwisho wa mwezi. Nikamshangaa sana huyu rafiki kwasababu yeye anazungumzia habari ya kukaa mahali mimi nawaza kufika mbali sana. Nikaona huyu sina haja ya kumweleza chochote maana atakuwa hanielewi kabisa.
Nataka ujifunze kwa watu wa aina hii wanaoona wewe uliemua kuanzisha biashara yako au kujikita kwenye ujasiriamali huku umeweka vyeti vyako pembeni wanaona kama vile unajitesa sana.
Ukweli mtu wa aina hii hana mawazo yeyote makubwa,
Ameridhika na kile anachokipata.
Hawazi kupata Zaidi ya ahapo anapopata.
Ni hatari sana kuwa na mtazamo wa huyu rafiki yangu kwani huu ndio ubinafsi ninaouzungumzia leo. Umezaliwa na vitu vikubwa ndani yako kukaa navyo mahali na kusema ni kutesa kufikia ndoto yako ni ubanafsi mkubwa sana. Kwasababu inawezekana dunia inasumbuka sehemu Fulani halafu wewe ndie uliezaliwa uje kusuluhisha hilo tatizo kama utakaa mahali useme wewe hufanyi chochote mshahara unakutosha ukuwa unaua uwezo ambao Mungu ameweka ndani yako.
Badilisha mtazamo wako kama na wewe una mawazo ya aina hiyo. Tukiwa na watu wengi wanaowaza kama rafiki yangu kamwe hatutaweza kuendelea kama nchi ama jamii ya mahali. Tunahitaji watu wengi wenye mawazo ya ubunifu ili kubadilisha hali mbaya zinazoendelea duniani.
Maisha ya wengi yatakuwa marahisi sana kama tutatoka sehemu zile ambazo tumezizoea kwasababu zinatutimizia mahitaji yetu na kwenda mbali Zaidi ili kufikia makubwa.
Toka sehemu uliyopo kama haikusababishi wewe uwaze makubwa na kukua kila siku.
Tunapaswa kuwa watu tunaotatua matatizo na sio tunaotengeneza matatizo duniani. Usikubali kuwa mmoja wa watu wanaowaza mawazo ya kula na kulala basi waza mbali Zaidi ya ulivyozoea kila siku.
Rafiki Yako,
Jacob Mushi
Asante sana