Mwaka 2003 nikiwa darasa la nne nilikua na tabia ya kusoma sana vitabu, magazeti na majarida ya hadithi za mapenzi. Vitabu vingi nilivyokuwa navisoma vilikua vya hadithi mbalimbali za kutisha na mapenzi. Magazeti  niliyokuwa nasoma yalikua ya siasa na ya udaku. Pia niliweza kusoma biblia agano la kale vitabu karibia vyote. Embu jiulize darasa la nne tayari nilikua na taarifa nyingi kichwani mwangu za kila namna. Darasani likiulizwa swali linalohusiana na Viongozi mbalimbali wa serikali nilikua wa kwanza kujibu.
Nilisoma vitu vingi sana vingine siwezi kuvitaja hapa. Kwa umri wangu mdogo nikajikuta nimebeba taarifa nyingi kichwani ambazo nyingine zisihitaji katika maisha yangu kwa ujumla.

?Taarifa zinawezaje kupofua Macho yako ya Ndani?

?Taarifa zisizofaa zinaharibu maono.

Maono yako ndio yanatokana na macho yako ya ndani, hivyo kama utakua unaingiza taarifa zisizoendena na kile unachokiona, mwisho wa siku utapoteza uwezo wako wa kuona maono.

?Zinaharibu Nguvu yako Ya kufikiri.
Kama ambavyo ukila vyakula vibovu vinakufanya uwe na afya mbovu, hivyo hivyo na taarifa zisizohitaji kwenye ubongo wako zinakuharibu. Uwezo wako wa kufikiria utapunguzwa kwa kadiri ya taarifa ambazo zipo kichwani mwako. Kama wewe unapenda kufaulu darasani unaambiwa uachane na mapenzi shuleni maana yatakupotezea uwezo wako wa darasani. Yaani ukijihusisha na mapenzi huku unasoma utajikuta unaelemea zaidi kwenye mapenzi. Ukizoea kula chips mara kwa mara baada ya muda utajikuta huwezi kula vyakula vyenye afya utapenda kula chips maana ni rahisi kupatikana.
Ukifuatilia zaidi taarifa za mambo mabaya yanayoendelea duniani unaweza kuona kama mwisho wa dunia ni kesho ukakosa hata nguvu ya kufanya Mambo mengine.

Akili yako Inafanya kile unachoiambia ifanye. Akili yako inafanyia kazi taarifa ambazo unazijaza kichwani mwako.

Taarifa mbaya zinapunguza kasi ya wewe kuzalisha.

Tuseme wewe Unatumia lisaa limoja kuangalia Tv kila siku,  lisaa limoja kutazama tamthilia au movie yeyote na masaa mawili kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii.  Jumla utakua Unatumia masaa manne kila siku. Haya masaa manne ukizidisha kwa siku 30*4=120hrs yaani wewe kwa mwezi mzima Unatumia masaa 120 kufanya hayo Mambo niliyoorodhesha hapo.

Masaa 120 ni sawa na siku tano. Yaani unapoteza siku tano kila mwezi  kwa kuangalia Tv na Mitandao ya Kijamii. Hizi siku tano ungeamua tu kuzigawa basi badala ya kuzutumia zote kufanya hayo mambo uwe unasoma kurasa moja ya kitabu au usikilize audio book moja ungekua umeongeza maarifa kiasi gani kichwani kwako?

Mwaka mmoja ungekua mtu wa namna gani?  Haijalishi uko bize kiasi gani tenga lisaa limoja la kusoma kitabu kila siku utaona maisha yako yatakavyokua ya tofauti.

Bonyeza hapa upate vitabu vya kusoma.

Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
An Author of a book called “Siri 7 za Kuwa Hai Leo “
Phone : 0654726668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading