#Hujamaliza Kazi.

Kila kitu kina sababu ya kuwepo kwake duniani mpaka leo.  Wewe pia uko duniani kwa sababu  hauko duniani kwa bahati mbaya.  Weqw kupumua leo ni sababu pia yapo mambo yanakupasa uyafanye. Je umeshatambua kwanini upo hai leo?

#HujamalizaKazi ndio Hujamaliza kazi uliyotumwa Kuifanya duniani. Na kama bado hujaitambua kazi mimi siweze kukuambia kazi yako rudi kwenye kile unachokiamini na kukisimamia utapata majibu sahihi rudi kwenye imani yako ya kiroho,  nenda kule unapokulia kiroho.  Miili yetu haiwezi kufanya kazi bila roho zetu roho ndiyo inaongoza mwili ukiisahau roho utajikuta kila unachokifanya duniani hakina furaha kabisa.
Hujamaliza Kazi ya kubadili dunia.  Dunia ulivyoikuta unatakiwa uache mabadiliko usiondoke bila kuacha mabadiliko yeyote hapa duniani. Huko unapokwenda utadaiwa kwa kuchezea nafasi uliyopewa hapa duniani.

#WakoWengiWamekufa tena ni wema zaidi yako lakini wewe unapumua unafikiri ni bahati mbaya?  Watoto wanazaliwa hospitali hwajafanikiwa hata kuona miti huku duniani wanafariki wewe upo hai bado unalalamika.  Kua Hai peke yake ni fursa kubwa sana.  Kuwepo siku ya leo ni Fursa kubwa mno usichezee fursa hii ya uhai ulio nao.  Nguvu ulizo nazo zitumie vyema kuleta mabadiliko katika ulimwengu huu.  Ulimwengu unakusubiri wewe ufanye na utajitokeza kukusaidia anza leo fanya fanya fanya fanya fanya.  Usiogope kama unaandika andika hadi kila mtu ajue unaandika kama unaimba imba hadi kila mtu ajue unaimba maana siku ukifa hautapata tena nafasi ya kufanya chochote zaidi itakua ni majuto ukiwa peke yako ndani ya jeneza.

#SasaHivi  Unawaogopa watu unajua ukifa unaondoka mwenyewe unaowaogopa watabaki aua watakufa kila mmoja kwa namna yake?  Usiogope wala kutetemeshwa na chochote wote tutakufa na tutaicha dunia fanya kile moyo wako unakipenda na fanya kwa bidii hadi uache mabadiliko makubwa kwenye dunia hii.

#KilaMmoja angetambua kwamba anatakiwa aache alama duniani  dunia ingekua ipo mahali pazuri sana kipindi hiki lakini hilo hatuwezi kulikulibadili tunachoweza kufanya ni yake ya kwetu yaliyotusababisha tuje hapa duniani.

#HujachelewaBado haijalishi una miaka mingapi sasa kama  upo hai na una ufahamu bado unaweza kufanya mabadiliko makubwa duniani.  Hata kama upo kitandani huwezi kutembea unaweza kurecord sauti na maneno yako yakaacha mapinduzu makubwa hapa duniani.

Swali langu la mwisho kwako. #UnatumiajeFursaHii ya uhai ulionao leo?

Jacob Mushi

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading