Kwa vyovyote vile hata kama utaogopa kufanya mambo yaliyo makubwa, hata kama utaogopa kupoteza pesa zako bado huwezi kuondoka duniani ukiwa hai. Kama unaogopa kupata msongo wa mawazo kwasababu biashara itakusumbua Rafiki yangu hata usipoupata huo msongo wa mawazo bado hapa duniani utaondoka ukiwa umekufa. Hatujui ni kitu gani kitakuondoa duniani hivyo basi wewe endelea kupambana usiseme naogopa kupata presha bure.

Usiseme hata nikizitafuta pesa bado nitaziacha ndio utaziacha lakini kumbuka hutaacha pesa tu utaacha na historia inayowapa wengine ujasiri na nguvu ya kuendelea kupambana.

Kile kilichopo ndani yako endelea kukisimamia bila kuogopa chochote, vikwazo visiwe sababu ya wewe kuogopa na kuacha. Bila kujali unapitia misukosuko ya aina gani wewe endelea mbele kwasababu hiyo ndio njia ambayo uliitiwa.

Usiogope kwamba kile unachokipigania ulimwengu mzima unakupinga bado inawezekana ukaleta historia mpya ambayo haikuwepo kabisa. Bado unaweza kuleta mapinduzi. Hakuna jambo kubwa ambalo lilianza kwa kukubalika na kila mtu. Mambo yote makubwa na watu wote wakubwa mwanzo wao ulikuwa ni wa kutaka kupotezwa na kupingwa na kila mtu.

Usiogope kifo, usiogope wanaokutisha kwasababu hata ukikaa chumbani bado utakufa. Hofu yako ni ya nini sasa? Kama usipofanya kile ulichoitiwa kuja kufanya utakufa na ukifanya utakufa unaogopa nini sasa? Chukua hatua maneno ya watu yasikutishe.

Kitu pekee ambacho unapaswa kukiogopa ni woga wenyewe.

Ukienda vitani unakuwa umekubaliana na lolote ambalo linaweza kutokea yaani kufa au kupona, lakini katika Maisha kufa ni lazima ufe lakini mafanikio ndio unachagua kuyapata au kuendelea kubaki hivyo ulivyo.

Hautaondoka hapa duniani ukiwa hai endelea kufanya kwa bidii hata uache alama kama mashujaa waliofia vitani. Ndoto yako inawezekana acha kuogopa, acha kuwasikiliza waliokata tamaa. Wasikilize waliofika mbali kuliko hapa ulipo sasa.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading