Mimi ni fundi wa kompyuta, inapotokea kompyuta ninayotumia imezima ghafla siwezi kukimbilia kwenda kubadili ule mfumo unaoendesha kompyuta nzima (windows). Hiyo inaweza kuwa ni suluhisho lakini kabla sijafanya hivyo lazima kwanza nianze kujua tatizo ni nini na limesababishwa na kitu gani. Kujua tatizo ndio kutanipa mwangaza wa suluhisho la aina gani linatakiwa.

Katika Maisha yako unaweza kupitia matatizo ya aina mbalimbali, unaweza kuishiwa fedha, unaweza kuingia katika madeni, biashara zinaweza kuyumba sana na kadhalika. Kabla hujakimbilia kutafuta dawa ya matatizo yako kaa chini ujiulize ni kwasababu gani hayo matatizo yanakujia. Achana na Shetani ndio ameyaleta au sijui una bahati mbaya au useme ni kawaida haya kila mtu anapitia. Hapana unatakiwa ujiulize maswali magumu kwasababu inawezekana unasema ni Shetani halafu kumbe ni wewe mwenyewe.

Anza kwa kutafuta chanzo cha tatizo kabla hujaleta dawa, tanki la linalovuja maji huwezi kuzuia maji yasiiishe kwa kujaza maji kila saa bali unatakiwa uzibe panapovuja. Kuna suluhisho nyingine unazichukua zinakuwa kama kujaza maji sehemu ambayo inavuja hivyo kila wakati utajikuta unarudi tena kuifuata ile suluhisho.

Tafuta kujua Tatizo limeanzia wapi, na sababu has ani ipi kisha uanze kujitafutia dozi ya tatizo lako. Ukiona unashindwa kabisa kujua chanzo ni kitu gani tafuta mtu ambaye unamwamini (Kocha au Menta) akusaidie.

Kama yalivyo magonjwa huwezi kupona ndani ya siku moja, huwezi kupewa dawa leo na ukapona leo, unaweza kupata nafuu lakini sio kupona moja kwa moja labda uwe muujiza. Hivyo pia katika kutatua matatizo yako usipende kupata utatuzi wa haraka kwasababu mara nyingi husababisha tatizo kujirudia. Kuwa mvumilivu chukua hatua ambazo umeshauriwa, rudi uliza maswali pale ambapo hujaelewa, unaposoma Makala kama hii ukaona hujaelewa muulize muandishi akusaidie Zaidi usikubali kuwa daktari wakati unaweza kusaidiwa kwa ushauri.

Usikubali kukimbiliakutafuta dozi wakati hujajua ugonjwa wako ni upi na unasababishwa na nini. Ninaaminiunaweza kuvuka tena kwenye changamoto unayopitia endapo utafuta utaratibu huumzuri wa kujua chanzo cha tatizo.

Habari njema kitabu cha USIISHIE NJIANI kimetoka katika nakala ngumu. Pata nakala yako popote ulipo Tanzania kwa tsh 7000 (elfu saba) tupigie kwa 0654726668.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Kocha Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading