Unapopitia magumu usiangalie magumu itazame ndoto yako.
Unapoona hupati kile unachokitaka kila wakati kila unapofanya vitu mbalimbali itazame ndoto yako.
Ukiona biashara haiendi vyema kama unavyopanga itazame ndoto yako.
Chochote kigumu unachopitia usikiangalie usiangalie ugumu itazame ndoto yako.
Kwanini nakwambia uitazame ndoto yako?
Unapoitazama ndoto yako utapata hamasa upya utapata nguvu mpya. Lakini haitoshi kuitazama peke yake. Jione ukiwa unaishi ile ndoto yako. Vuta taswira uone upo na ile gari ya ndoto yako unaendesha. Vuta taswira uone una kila kitu unachokitaka kwenye maisha yako.
Kiukweli huwezi kukata tamaa nguvu zitakurudia upya.
Tatizo kubwa wengi hukata tamaa na kurudi nyuma pale wanapoyatazama matatatizo badala ya ndoto zao. Ukiyatazama matatizo kwa mtazamo wa ugumu na kushindwa utakwama.
Anza leo kuitazama ndoto yako.
Una ndoto?
Umeshajua cha kufanya ili uifikie?
Kama bado au huna uhakika na kile unachokifanya tafadhali tuwasiliane nikupe mwongozo.
Karibu sana
Mwandishi:Jacob Mushi