Habari ndugu msomaji wetu ni wakati mwingine wa kupeana mbinu nzuri juu ya kuboresha biashara zetu kwa njia ya mtandao, leo tunaangalia jinsi ya kubadili biashra zetu kua za kiteknolojia.
Kama tunavyoona mabadiliko makubwa kwenye upande wa teknolojia kila siku mambo mapya yanatokea ni wakati wako sasa na wewe mjasiriamali kubadilika la sivyo utaachwa nyuma sana na hatimae biashara kufa au kubakia ya kawaida.
Ufanyeje sasa?
Kwanza kama umeweza kusoma Makala hii tayari upo kwenye njia salama, kitu cha kufanya ni kuchukua hatua. Chukua hatua sasa kama bado hujamiliki blog yako anza sasa kumiliki tutakutengenezea, kama bado hujajua jinsi ya kutafuta soko kwa njia ya mtandao wa internet tutakushauri Moja Technologies Group tupo hapa kuifikisha biashara yako mahali unapotaka ifike.
Miliki blog, kwa kumiliki blog utakua na uweze wa kuelezea kile unachokifanya kama wewe una kipaji chochote ifikie jamii kwa njia ya blog, biashara yako unayotamani iwafikie watu wengi Zaidi miliki blog, ujuzi ulio nao unatamani ufikie jamii miliki blog. Hii itakuwezesha kuweka historia ya kile ulichokianzisha.
Miliki kurasa za mitandao ya kijamii inayotembelewa na watu wengi kwa wenye biashara miliki kurasa yenye jina la biashara yako, ili kutangaza jina la biashara  hiyo, kwa kuanza unaweza kuona ni kazi nzito isiyo na matunda lakini kadiri unavyozidi kuwepo utajenga wateja wa kudumu na wanaokuamini.
Hakuna matokeo ya ghafla kwa kua umeanza leo uanze kupata wateja leo, inahitaji uvumilivu kwa mwanzo biashara inapokua imetambulika vyema wateja watakua wanakuja wenyewe.
Ni kwambie kwamba hakuna kinachoshindikana bado unayo nafasi ya kufanya mambo makubwa mabadiliko yanakuja tunatakiwa tuende na mabadiliko la sivyo tutaachwa nyuma.
Kwa msaada/ushauri tuandikie email mojatechnologiesgroup@gmail.com

Asante sana Sisi ni washindi.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading