Habari mpenzi msomaji wa makala zetu. Ni uhakika wangu kuwa uko vizuri kabisa. Hata mimi pia hadi wakati huu ninapoandika makala niko njema kabisa. Hili ni jambo la kumshukuru Mungu wetu. Leo katika mfululizo wa makala zetu nimependa kuja na swali hili, “IKO WAPI NDOTO YAKO?”
Kama unavyojua sote tulizaliwa na ndoto/maono ya kufanya au kuwa na kitu fulani, lakini kadri siku zinavyokwenda zile ndoto zinapotea taratiibu. Mfano, tukiwa wadogo kabisa wengi wetu tulitengeneza magari kwa kukata galoni, tukatumia tairi za malapa, kama sio magunzi, wengine waliona wasishindwe kabisa wakatengeneza hata baiskeli za miti.
 Unazikumbuka betri za ABC? Tuliziponda ponda ili tupate tairi! Wengine tulikuwa ni mainjinia wa ujenzi, tulitumia matope kujenga nyumba tena za kifahari kama sio ghorofa. Hakuna aliekubali kushindwa. Tulikuwa na malengo ya kuwa na familia bora, ya kuoa na kuolewa. Hahah! Kibaba baba na kimama mama. Michezo yote hiyo ilikuwa ni kama unabii wa kutimiza ndoto zetu.
Tulikuwa na ndoto za kuwa wahubiri/wachungaji, waalimu, n.k. lakini leo WHERE IS OUR DREAM? Hebu fanya tathmini kile ulichokuwa unakifanya ukiwa mtoto kimeenda wapi? na kwanini tumeshindwa kukitimiza? Halafu chukua hatua madhubuti. Pengine kukosa ajira na ugumu wa maisha kumefuta ile ndoto ya kumiliki gari. Au ni watu wamekuambia kama baba yako alikufa hana hata baiskeli wewe utakuwa na gari kweli? Au wamekuambia kuwa “huwezi” na wewe ukakata tamaa kabisa?
Kuzalia nyumbani kwenu kumeondoa ndoto yako ya kuwa mama bora wa familia? Ukaona huwezi tena kuolewa ukaamua kujiingiza kwenye ukahaba kabisa.? Kuishi kwenye nyumba ya kupanga na kukosa hata kakiwanja kumefuta ile ndoto yako ya kumiliki ghorofa? Je ni TCU walibadili ndoto yako pale ulipotaka kuwa daktari wakakupangia ualimu kwa sababu wewe ni mtoto wa mkulima? Hebu fikiria kingine tena. Ulikuwa na lengo la biashara lakini kuona mwenzako kaanza biashara uliyokuwa unaiwaza ukakata tamaa, na ndoto yako ikaishia hapo? Jifunze kwa YUSUFU katika biblia.
Licha ya kupitia changamoto nyingi ambazo zingeweza kuizima ndoto yake hakukata tamaa. Alitambua kuwa kupitia changamoto zote hizo MUNGU aliyakusudia kuwa ni mema. Soma mwanzo 50:20. Mwishowe anakuja kuwa waziri mkuu katika nchi ile ya misri. Nataka ufahamu kuwa kizuizi kikubwa cha ndoto zako ni wewe mwenyewe. Jitahidi ukiondoe kikwazo hicho. Utaitimiza ndoto yako. Usihesabu pale uliposhindwa. Jitie nguvu inuka tena kwani unaweza. Dont look back look foward always. Ninapomalizia naomba nikukumbushe mambo haya machache yatakayosababisha uzitimize ndoto zako.
 1. Usimkilize mtu yeyote anaekuambia kuwa huwezi, hata kama ni mtu wako wa karibu.
2. Weka malengo kutimiza ndoto yako
3. Itangaze ndoto yako na chukua hatua kuitimiza.
 4. Kila jambo unalolifanya mtangulize MUNGU kwani yeye ndio kila kitu. Nimalizie kwa kukuambia hivi, ‘YES. YOU CAN.
”OUR SUCCESS IS YOUR SUCCESS” 
Mwandishi: Steven I. Mshiu
0655882074 
smshiu42@gmail.com 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading