Katika Biblia vitabu vya Injili tunamwona Bwana Yesu akitenda miujiza kwa kuwaponya vipofu, viwete,na wenye madhaifu ya aina mbalimbali. Siku moja mwanamke alietokwa na damu kwamiaka 12 alipoamua kwenda kulishika vazi la Yesu akiamini kwamba ataponaalipona kweli. Yesu akamwambia Imani yako imekuponya. Ni kweli Imani yake NdioIlimponya.

Tukiangalia nyuma kabla hajaamua kwenda kumshika Yesu alikuwa ameshapitia kwa wanganga wa kila namna na hakupata msaada wowote. Kwenda kwa mganga hakwenda tu bila ya Imani, popote pale alipojaribu kwenda alikuwa na Imani ndani yake. Lakini zote hizo hazikumsaidia.

Inawezekana wewe Imani ambayo uliyojijengea ndio inakufanya uendelee kuwa na hali mbaya mpaka sasa. Hali mbaya ya kiuchumi, hali mbaya kwenye mahusiano, hali mbaya kwenye ndoa, hali mbaya kazini. Hii yote ni kwasababu kuna Imani umejenga na Imani hiyo ni potofu ndio maana unateseka.

Njia pekee ya kutoka kwenye Imani hiyo ni wewe kutambua kwamba kile unachokiamini hakifai, ulidanganywa au ulikuta wanadamu wenzako wanaamini na wewe ukaendelea kushikila hivyo hivyo bila hata kujiuliza chochote.

Inawezekana ulidanganywa kwamba huwezi kuwa Tajiri bila kuiba ndio maana huhangaiki kutafuta pesa wala kuweka bidii kwasababu unaamini kwamba ili uwe Tajiri lazima uibe tu.

Inawezekana mahusiano yako ni mabovu kwasababu ulidanganywa au tunasema uliaminishwa kwamba wanaume wote wana tabia moja au wanawake sio watu wakuwaamini kabisa. Hii imekufanya uwe na migogoro kwenye mahusiano kwasababu humuani na yeye hakuamini.  Huenda pia uliambiwa kabila la huyo ulie nae hawafai wana tabia mbaya na wewe umekuwa unaishi kwa Imani hiyo na hivyo kuendelea kuteseka kila analofanya hata dogo unasema “hawa watu hawafai kabisa niliambiwaga sikusikia”.

Inawezekana hapo kazini unapofanya kazi uliaminishwa kwamba bosi ni mshirikina hivyo umekuwa ukipata mshahara unaisha haraka unafikiri labda ni bosi anaurudisha kimazingira kumbe ni matumizi yako mwenyewe mabovu.

Hizo ni baadhi ya Imani ambazo unaweza kuwa umejengewa sehemu mbalimbali kwenye Maisha yako na zinakutesa bila wewe kujua na wakati mwingine unajua kwamba unateseka. Ili uweze kuziondoa Imani hizo ni lazima kwanza ujitambue, uhitaji msaada  maana mganga hajigangi, mchezaji hajifundishi mwenyewe, unahitaji mtu akusaidie uondoe kabisa hizo Imani uanze upya ujenge Imani mpya na ubadilike.

Anza sasa kutengeneza Imani ambayo itakusaidia, futa Imani zote potofu ndani yako ulizojengewa. Tengeneza Imani ambayo itakusaidia na kukufanya uwe mtu bora Zaidi.

Jiunge nami katika program ya mwaka wa mafanikio ili uweze kujenga Imani mpya za mafanikio katika Maisha yako. Bonyeza link mwishoni mwa Makala hii.

Ubarikiwe sana,

RafikiYako,  Kocha Jacob Mushi

4 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading