Imetosha kuendelea kuwa mtu wa kawaida, Imetosha Kuendele kuitwa maskini.

Imetosha kuendelea na hali ile ile ya Maisha kila wakati. Ulisemwa hauwezi kufanya chochote kwasababu umefeli shule imetosha. Walisema wewe hujawahi kufanya jambo lolote la maana imetosha sasa.

Ni wakati wako wa kufanya maamuzi ambayo hayana kurudi nyuma tena, ni wakati wa kuamua kuweka historia ambayo vizazi na vizazi vitakuwa vinajifunza kwako. Ni wakati wa kufanya jambo ambalo litakuja kuandikwa kwenye vitabu kama mfano.

Sio wakati wa kukubaliana na maneno yao, ni wakati wa kuchukua hatua. Rafiki yangu unafikiri ni lini sasa utaanza kufanya kile ambacho umekuwa unasema utafanya? Ni sasa, ni leo, anza kidogo kidogo, fanya kila siku.

Ukiamua kuweka historia kwenye kuandika andika kila siku hadi dunia ijue wewe ni mwandishi. Ukiamua kuweka historia kwenye uimbaji imba hadi watu waseme haijawahi kutokea sauti nzuri kama hii duniani. Amua kuweka historia mpya sasa, yote waliyoyasema yatabaki kuwa kweli kama hutaamua kuchukua hatua.

Kama wewe bado hujaona kama imetosha endelea kusubiri ila nakwambia wakati sahihi ni sasa. Hakuna mtu mwingine atakuja akusukume utoke hapo ulipo kama hujaanza kufanya chochote.

Unajua hata kama umezama mtoni kwenye maji watu wanaweza kuja pembeni yako na wasijue kama upo endapo hutakuwa unaonesha jitihada zozote za kujiokoa hata kwa kupiga kelele tu. Usipofanya kitu watu waone na wajue kama upo watakusahau na utapotelea kwenye maji.

Endelea kupiga kelele, endelea kujaribu kujiokoa hapo ulipozama hutajua ni nani atasikia kelele zako. Usiogope kama nguvu unazo zitumie hizo, chochote kile ambacho unacho kitumie kama njia ya kujiokoa na kufikia mafanikio.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Kocha Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

2 Responses

  1. Nakushukuru sana unanifanya nisiwe naka tamaa japo mapito yamezidi namwomba mungu anisaidie niweze kufikia malengo yangu.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading