Iwapo ukiambiwa kesho ndio itakuwa ni siku yako ya mwisho hapa duniani unafikiri ni vitu gani hasa ungevifanya leo?

Embu viandike vitu hivyo basi uwe unavifanya kila siku.

Unafikiri ni nani ungeongea nae kwa simu na kumuaga?

Embu endelea kuongea nae kila siku.

Unafikiri ni nani ungetaka umwonyeshe kuwa unampenda kwa dhati?

Embu mwonyeshe kila siku.

Unafikiri ni nani ungemwomba msamaha kwa makosa ambayo ulimfanyia na hajajua?

Embu mwombe msamaha leo maana hakuna ajuae kesho.

Ishi leo kwakuwa leo ndio pekee tulio na uhakika nayo. Usibaki unasema nitaonyesha upendo nikiwa na hela hapana.

Usiseme ukiwa na vitu Fulani ndio utafurahia Maisha kama umeshindwa kufurahia Maisha kwa kidogo ulichonacho hata kikubwa utashindwa.

Leo ndio siku ya pekee ambayo unatakiwa uitumie kufanya yale ambayo unatamani yabaki kama alama hapa duniani.

Kama kuna wimbo ulitamani kuuimba uimbe sasa, kama kuna kitabu unatamani kuandika kiandike sasa.

Kuna nyakati zitafika hutaweza kufanya tena yale uliyokuwa unataka kuyafanya. Kuna nyakati zitafika hutakuwa na sauti nzuri uliyonayo sasa hivi.

Maisha ni kama kifurushi kuna wakati kina expire, kuna nyakati zitafika utakuwa una mambo mengi ya kufanya na nafasi huna.

Kuna nyakati zinakuja hutakuwa na nguvu ulizonazo sasa hivi.

Muda hauna huruma, muda hautazami wewe ni maskini au tajiri.

Muda hautazami wewe ni mgonjwa au ni mzima.

Muda hautazami changamoto unayopitia sasa hivi eti ukusubiri.

Muda unakwenda mbele. Hivyo ni vyema kufanya yale yanayowezekana sasa hivi tukiwa na nguvu na yale yasiyowezekana tutafute namna ya kuyafanya yawezekane.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading