Inawezekana kwenye uko wenu familia yenu ndio mna hali duni kuliko wengine wote na hivyo kuonekana kama mnawategemea wale ambao wamewazidi.

Inawezekana umefeli masomo na hujaweza kufikia elimu ya juu ambayo uliambiwa ndio mkombozi wa Maisha yako.

Inawezekana pia umezingirwa na madeni makubwa sana hadi aibu na wakati mwingine unashindwa kupita hata mtaani.

Inawezekana unaonekana wewe huna uwezo, umedharaulika kutokana na aina ya Maisha uliyonayo na umeshakata tamaa kabisa.

Inawezekana unategemea muujiza Fulani uje ukutoe kwenye hali hiyo unayopitia sasa hivi. Ukweli ni kwamba kama sio kusudi la Mungu wewe uwe hivyo haiwezekani ukatokea muujiza wowote. Kama hali unayoipitia haijasababishwa na mleta muujiza usitegemee muujiza.

Kama hali ambayo unapitia inatakiwa kuondoka kwa kuweka juhudi na maarifa usitegemee muujiza.badala ya kukaa na kungojea kitu kije kitokee chenyewe cha ghafla na kubadilisha kila kitu anza wewe kuchukua Hatua sasa.

Usijitie moyo kwamba Mungu yupo na ananiona. Ukweli ni kwamba wapo watu miaka na miaka iliyopita walikuwa wanapitia hali kama zako na wakabaki nazo hadi wanakufa. Kama mungu hajakuletea hiyo hali unatakiwa ujue unahitaji juhudi za ziada kutoka hapo ulipo.

Sisemi kwamba usitegemee chochote kwa Mungu la hasha, wewe muombe Mungu akuongoze katika kila unalotaka kufanya. Lakini usibaki unamsubiri wakati hajakwambia umngoje kwenye hali uliyonayo. Anza sasa kuchukua Hatua kwasababu hiyo ndio njia pekee watu waliokuwa wanakusema wataulizana na kushangaa, matokeo ya juhudi na maombi yako kwa Mungu yatakapoleta majibu.

Ni vizuri sana kukaa na Mungu vizuri ili akuonyeshe kule unapokwenda kunahusiana vipi na hali unayopitia. Ile sehemu ambayo unapaswa kukaa kimya ukae kimya usubiri yeye ajibu, ile sehemu ambayo wewe unapaswa kukimbia ukimbie na uchukue Hatua.

Hata Daudi aliweza kupata nafasi ya kumpiga Goliathi baada ya kupeleka chakula kwa ndugu zake kule vitani. Kama asingekwenda akabaki kuchunga kondoo asingeweza kulitimiza kusudi lake. Kuna sehemu unatakiwa uwepo ili uweze kukutana na muujiza wako. Kama unatakiwa kuumua Goliathi basi nenda vitani usikae shambani kuchunga kondoo wakati wote.

Ili watu waulizane lazima jitihada zifanyike. Ili watu washangae lazima uchukue Hatua Fulani za kufanya matokeo kwenye Maisha yako.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading