Kuna nyakati kwenye maisha tunapitia hali ambazo zinatulazimisha kufanya mambo tusiyohitaji ila ni kwasababu tunaisikiliza mili yetu. Sio kila hali ambayo unaisikia kwenye mwili wako inahitaji kufanyiwa kazi.

Ukiwa na mtoto mdogo utaweza kuniambia kwamba sio kila anacholilia mtoto unampatia. Mfano anatakiwa kulala na yeye anataka kwenda kucheza huwezi tu kumruhusu kwasababu ametaka.

Anatakiwa kula chakula akalilia soda huwezI kumpa soda kwasababu tu amelilia.

Mara zote tunawapatia watoto wetu vile vitu wanavyostahili na sio kwa vile tu wamelilia.

kwenye maisha na safari ya mafanikio kuna nyakati utataka kufanya mambo na mwili wako ukakataa. Kuna nyakati unatakiwa usome vitabu lakini unajisikia uvivu.

Kuna nyakati unatakiwa ukamilishe jambo fulani lakini mwili unakwambia umechoka utamalizia kesho.

kama utausikiliza mwili wako na hali zake utajikuta hakuna unachokifanya. 

kama kila unavyojisikia wewe unafanya utajitengenezea tabia ambazo zinaweza kuwa sababu ya wewe kukwama kwenye safari yako.

Lazima ujue ni vitu gani lazima ufanye bila kujali una usingizi au lah lazima ujitengenezee nidhamu kama mtoto mdogo.

 

Jacob Mushi.

USIISHIE NJIANI

0644726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading