Ili uweze kua na ubunifu na uvumbuzi bora lazima ukubali kujifunza. Lazima uipe akili yako chakula ili iweze kukuzalishia matunda bora. Ili ng’ombe atoe maziwa bora anapatiwa majani ya kutosha pumba nzuri na maji ya kutosha. Ukijisahau hujampatia chakula huwezi kupata maziwa ya kutosha kwa ng’ombe. Ilishe chakula bora akili yako ikupatie matokeo bora.
Jifunze kwa waliokutangulia jifunze kwa walioko mbele yako, jifunze kwa kila mtu unaekutana nae. Kila unaekutana nae ana kitu cha kujifunza kwako na wewe una kitu cha kujifunza kwake. Hivyo basi ni wakati wako wa kujifunza kwa kila unaekutana nae. Usikubali kufunga mlango kuzuia kitu kipya kwenye maisha yako utakua kwenye hatari ya kubakia katika hali uliyonayo kila siku.

Jifunze kupitia vitabu, kama unataka kua mbunifu na mvumbuzi lazima ukubali kusoma vitabu. Kwa kupitia vitabu utajifunza mbinu nyingi za kukuwezesha wewe kutoka sehemu ulipo na kufika sehemu ya juu Zaidi. Usikubali kuicha akili yako hovyo hovyo tu hakikisha kila kinachoingia kina manufaa. Jiulize unaweza kulisha tumbo lako chakula kichafu? Lazima utaumwa na tumbo! Kwanini ukubali sasa kuingiza taka kwenye akili yako? Chagua cha kuweka kwenye akili yako.

Hudhuria semina hakikisha unahudhuria semina mbalimbali za mafunzo huko utakutana na watu wenye upeo wa tofauti na utaweza kujifunza kwao. Embu jiulize mara ya mwisho kuhudhuria semina ilikua ni lini?

Zama hizi za teknolojia njia za kujifunza zimekua rahisi sana unaweza kuingia darasani kwa kupitia simu yako ya mkononi. Unaweza kusoma kitabu kupitia simu yako ya mkononi. Huwezi kujitetea kwamba umekosa nafasi ya kujifunza kila kitu kipo mkononi mwako unaweza kutumia vyema au ukaharibu.

Sikiliza audio books, siku hizi hata kama unasema wewe ni mvivu kusoma au huna muda wa kutosha kukaa ukisoma vitabu kuna audio books zimeshasomwa tayari unaweka kwenye simu yako unasikiliza au unaweka kwenye gari. Ukileta sababu ni wewe mwenyewe maana njia za kujifunza zimekua rahisi sana. Ukiamua kua mjinga ni wewe umeamua kwa kua maarifa yapo kila mahali. 

Karibu sana
Siri 7 za Kuwa Hai Leo
Jacob Mushi
0654726668
jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading