Kabla wengine hawajaona kilichopo ndani yako ni vizuri zaidi ukawa wa kwanza kukiona na kukijua vizuri.

Kabla wengine hawajaanza kukusifia jisifie Mwenyewe  na hapa simaanishi mbele za watu hapa ni wakati ukiwa Mwenyewe chumbani.

Kabla wengine hawajakwambia unaweza anza kujiona unaweza, jiambie naweza jione ukiweza jione ukipiga hatua mbele Zaidi.

Wewe ni mtu wa pekee sana anza sasa kuona nguvu uliyonayo, uwezo ulionao,  akili ulizonazo,  fursa zilizokuzunguka na uzitumie kukuletea mabadilko na maisha bora zaidi.

Maisha ya mafanikio yanafikiwa na hatua ndogo ndogo tunazopiga kila siku usidharau kile kidogo unachokifanya kwani kina mchango mkubwa sana kwenye maisha yako.

Napenda kukutia moyo kwamba hakuna kisichowezekana ni wewe kuamua na kuanza kutumia uwezo  uliopo ndani yako.

Kama unapitia changamoto ni muda wa kukaa chini na kuandika unachokipata kwenye changamoto hizo.  Lazima utoke wa tofauti kwani  utakwenda kupanda viwango.

Ni wakati wako sasa kujiamini, kujikubali na kuanza kuchukua hatua kusonga mbele, songa mbele hadi ufikie kile unachokitaka.

Kila kitu kinawezekana ndoto ulizonazo zinaweza kutimia usikate tamaa wala kurudi nyuma.

Kujifunza fursa za biashara wasiliana nami kwa no zangu mwishoni.

Karibu sana
Mwandishi: Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading