Habari za leo ndugu msomaji. Ni matumani yangu kwamba unaendelea vyema na mapambano katika kuifikia ndoto yako. Ni kweli kabisa unaweza kuifikia ndoto yako na mimi kazi yangu ni kukupa njia na vitu vya muhimu vya kufanya ili ukifika kule unakoenda udumu. Leo tunaingalia tabia ya Shukrani ambavyo inaweza kutumika katika kumwezesha mtu afikie mafanikio makubwa.

Shukrani ni nini?
Kwa kiingereza tunasema gratitude (the quality of being thankful; readiness to show appreciation for and to return kindness.ni ile tabia ya kusema asante kuonyesha kujali, kuthamini na kukubali kitu/mchango ulichokipata kwa yule aliekupatia. Kila mmoja wetu haijalishi upo kwenye hatua gani hii tabia ni ya muhimu sana kwenye maisha yetu. Kujenga tabia ya shukrani kwenye maisha yako kunakuwezesha sana wewe kufungua njia nyingine za mafanikio. Mtu anapokua amechangia chochote kwenye maisha yako unatakiwa ujijengee tabia ya kusema asante. Wako wengine watakuumiza lakini watakufundisha. Unaposema asante unamfanya yule aliekupata mchango aone umemjali na umethamini kile alichokupatia hivyo mara nyingi hawezi kuishia hapo. Akikutana na kingine kizuri atakuletea.
Anza kuonyesha shukrani kwa Mungu aliekuumba na kukuweka sehemu nzuri kama hii hapa duniani ambapo unafurahia maisha na wengine. Mungu amekupa uzima. Amekulinda hata leo bado unaweza kusoma hapa. Mshukuru Mungu kwa watu wema wote wanaofanyika Baraka kwenye maisha yako. Yako mambo mengi mno ya Kusema asante kwa Mungu wetu.

Washukuru watu wote wanaofanyika Baraka katika maisha yako. Hadi hapo ulipofikia sasa kuna watu wengi mno wametoa michango yao kwa namna mbalimbali. Wazazi wako, jamii iliyokuzunguka, waaalimu, dini yako, waandishi wa vitabu ulivyosoma, waandishi wa Makala kama hizi, Hua unafanya nini kuonyesha shukrani kwa kile unachopokea? Haijalishi mtu amechangia kidogo kiasi gani kwenye maisha yako kusema asante ni muhimu sana kwakua hujui ni nini kitakuja tena kwako kesho.
Yanapokukuta mambo magumu na mabaya maisha ni mwako ni wakati wako kutafuta jambo zuri la kushukuru badala ya kulalamika na kulaumu. Unapolalamika na kulaumu unajijengea ukuta wa kupokea mazuri, unapotafuta mazuri ya kushukuru unafungua milango ya kupata mengi Zaidi.

Jifunze kushukuru kwa mambo madogo unayopata. Usisubiri eti hadi upate makubwa ndipo uonyeshe shukrani. Tafuta muda ukae chini na uandike watu ambao unaona wana mchango mkubwa sana katika maisha yako na uwaandikie ujumbe wa kuwashukuru. Waambie kwamba umeouna na unathamini mchango wao kwenye maisha yako.

Tabia hii itakupeleka mahali pazuri sana. Watu wametoa sehemu ya maisha yao kwa ajili yako ili wewe uendelee vyema ni vizuri sana kuonyesha shukrani. Mtu anaekupa hata dakika moja ya maisha yake ni wa thamani sana.
Develop an attitude of gratitude, and give thanks for everything that happens to you, knowing that every step forward is a step toward achieving something bigger and better than your current situation. Brian Tracy
Jijengee tabia ya shukrani na kusema asante kwa kila kinachotokea kwako, tambua kwamba kila hatua ni hatua ya kupata kitu kikubwa Zaidi ya hapo ulipo sasa. Brian Tracy.
Sema asante kwa kila linalotokea kwenye maisha yako hata kama ni baya sema asante maana limekuja kukufundisha kitu.

Maneno yangu ya mwisho kwako ni haya… “Unaweza, Hakuna wa kukuzuia wewe, Unaweza kuitimiza ndoto yako. Ninazungumza haya kutoka moyoni mwangu. Unaweza na Hakuna wa kukuzuia. “

Usisahau kujiunga nasi  bonyeza hapa 
Karibu sana
Siri 7 za Kuwa Hai Leo
Jcobtz@gmail.com
0654726668
Jacob Mushi.

3 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading