Habari za leo ndugu yangu. Natumaini unaendelea vyema katika mapambano. Leo nataka tukajifunze tabia ya Uaminifu ambayo inaweza kukusababishia wewe uendelee kupata fursa nyingi kila siku. Uaminifu ni nini? Kwa lugha ya kiingereza tunaweza ni maneno loyalty, fidelity kutekeleza wajibu wako na kile ulichokiahidi kwa usahihi inawezekana ni kwa rafiki yako, mpenzi wako, mke, kazini, kwenye dini yako, na kadhalika. Tabia hii ndio karibia kila sehemu utasikia watu wanatafutwa, kazini utasikia tunatafuta mtu mwaminifu, kwenye mahusiano pia wanatafutana watu waaminifu, marafiki vile vile wanatafutana wanao aminiana. Kama huna tabia hii ya uaminifu utakua unakosa vitu vingi sana katika jamii yako.
 
Uaminifu unakuleteaje fursa? Kama wewe una tabia mbovu mbovu katika jamii itachelewa sana kufanikiwa kwasababu kila inapotokea fursa au dili kama wanavyoita, hutaweza kuitwa. Labda una tabia ya utapeli unakopa pesa za watu na hurudishi kwa wakati au unapotea nazo kabisa. Haiwezekani ikatokea kazi ukaitwa au ukapewa. Nakumbuka miaka kama mitano iliyopita nilikua nafanya kazi za ujenzi kama kibarua. Mara nyingi nilikua naona mafundi waaminifu ndio wanaopata kazi nyingi kuliko wale wanaodanganya. Hata wale vibarua wenye tabia ya uaminifu walikua wanapendelewa Zaidi kuliko wale wanaojulikana na tabia mbaya.
Haiwezekani ukipewa kazi na mtu unajikuta unatamani wewe ufaidike kuliko kile unachotoa. Uaminifu unajengwa na vitu vidogo vidogo sana tunavyofanya kila siku. Watu wanakutazama sana kuliko wewe unavyojua. Kuna mambo madogo madogo unayafanya kila siku na yanakujengea picha mbaya sana mbele za watu hivyo unajikuta unakosa mambo mazuri sana ambayo ungetakiwa uyapate.
Simu zetu zimekua sumu kubwa sana katika kuharibu uaminifu wetu watu wanadanganya kupita maelezo. Wakati mwingine ni bora ukose kitu kwa uhalali kuliko kukipata kwa kudanganya. Haijalishi hicho kitu kinakwenda kukusaidia vipi maishani lakini kama umetumia uongo kukipata kina madhara makubwa sana katika maisha yako.
 
Uaminifu kwenye Mahusiano
Hii ni sehemu ya kua nayo makini sana maana inaweza kukuharibia kabisa maisha yako ya baadae kama umezoea kutoka nje ya ndoa utajikuta ni tabia ambayo itakuja kukuaibisha sana huko baadae usisubiri aibu acha mara moja. Yale unayomfanyia mwenzako jiulize kama ni wewe unafanyiwa hivyo utafurahia? Ukija kugundua na mwenzako anakusaliti utafurahi? Kama kuna unachokikosa kwa mwenzako ni vyema kukaa chini pamoja na kuwekana wazi ili kurekebisha. Tabia ya kutokua mwaminifu kwenye mahusiano inaweza kukuharibia hata kazi au future yako ya baadae. Jiandae sasa kwakua hujui kesho yako inakwenda kua vipi. Na sio kwa ajili ya kesho tu ila ni kwasababu ni tabia uliyoamua kuishi. Ukitaka kuaminiwa anza kua mwanimifu. Tekeleza kile ulichokiahidi kwa mwenzi wako au mchumba wako. Ukitaka mpenzi mwaminifu anza wewe kua mwaminifu atakuja alie mwaminifu kwako.
 
Uaminifu kwenye biashara.
Kwenye biashara hapa ukikosa uaminifu unapoteza faida, unapoteza wateja , unapoteza hata jina lako. Tekeleza kile ulichokiahidi kwa mteja wako. Umesema bidhaa yako itamfanyia hiki. Hakikisha kweli inafanya. Ukiwa mwaminifu kwenye biashara unatengeneza hata wateja usiowajua. Hakikisha umefahamu kwa undani mteja wako anahitaji nini ili uweze kumridhisha. Kama hujajua anataka nini mteja wako huwezi kumpatia na kumfanya arudi tena.
Unampokeaje mteja anapokuja kwenye biashara yako? Kuna sehemu ukienda kununua kitu hautamani kurudi tena kutokana na mapokezi yao yalivyo mabovu. Kwenye matangazo unakuta wameandika tunakujali mteja lakini ukifika wanakupokea kama mwenyeji. Kwenye zama za sasa unatakiwa ujue kwamba haupo peke yako na unapokosea kidogo mtu anakwenda kwingine.  Mfanye mteja wako ajione kama ndio ameanza kuja leo kwenye biashara yako. Tekeleza kile unachoahidi kwa wateja na wafanyakazi wako.
 Mabosi mara nyingi tunajisahau sana. Kuna sehemu nilishawahi kufanya kazi Mkurugenzi hawajali wafanyakazi anawafanya waishi kwa hofu na kila wamwonapo wanakua kama wanatetemeka. Hii haifai sehemu ya kazi sio sehemu ya kukosa Amani kwa mfanyakazi. Mfanyakazi anatakiwa afurahie kazi yake ili aweze kumhudumia mteja wako vizuri. Bosi unatakiwa umjali mfanyakazi wako ili mfanyakazi wako amjali mteja. Vile unavyomfanyia mfanyakazi wako ndivyo anavyowafanyia wateja wako. Hata sasa tunaona yanayoendelea nchini. Kama sehemu ya kazi inakua ni sehemu ya hofu hakuwezi kua na uzalishaji bora. Bosi tekeleza kile ulichoahidi kwa wafanyakazi wako.
 
Uaminifu kwenye Kazi.
Umeajiriwa unatakiwa ujue ulichoahidi kwenye kazi yako ni kipi na ukitekeleze kwa uaminifu, kufanya kazi kwa bidi na ubora. Ukishindwa kua mwaminifu kwenye kazi huwezi kupata mambo mazuri. Ndio maana ukiacha kazi sehemu ukaenda kuomba kazi sehemu nyingine unaulizwa kwanini uliamua kuacha kule lengo sio tu kujua ni kitu gani ulikua unakosa pia kujua wewe una tatizo gani. Maana inawezekana uliacha kazi kwasababu wewe ni mvivu, sio mwaminifu, na kadhalika. Tekeleza ulichoahidi fanya kazi kwa furaha.
Tunajua kabisa watu wanatazama yale tuliyofanya nyuma lakini hiyo haina nguvu sana kama utaamua kubadilika leo na kuwa muamininifu  katika zile sehemu ambazo umekua unadanganya. Haijalishi ulikosea kiasi gani ukiamua kubadili leo tabia zako unaweza kufikia mafanikio.
 (credibility- the quality of being trusted and believed in.) ili uweze kujijengea kuaminika unatakiwa uanze kua na tabia ya uaminifu kwanza. Ili mtu aanze kukueleza mambo yake ya ndani kwanza anaanza kukuamini. Inawezekana kabisa ulikua na tabia ambazo hazifai huko nyuma. Huwezi kubadilia historia hii. Unachoweza wewe ni kuanza sasa kuishi katika tabia ambazo zinakuletea mafanikio katika maisha yako.

Huwezi kufikia mafanikio makubwa kama unatabia ya udanganyifu, tabia ya uaminifu ndio inaweza kukupa wewe nafasi ya kufikia mafanikio makubwa na kuitimiza ndoto yako. Hivyo jiangalie mara mbili mbili je unataka ndoto yako itimie? Una tabia ya Uaminifu? Kama hunaanza kuiejenga leo. Huo ni ukweli watu hawawezi kukupa fedha zao kama huna uaminifu ili uwe bilionea kuna thamani unitoa kwenye jamii na jamii ndioinakupatia pesa kama huna tabia ya uaminifu hakuna wa kukupa pesa. 

 

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

3 Responses

Leave a Reply to Baraka asajileCancel reply

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading