Habari za leo Ndugu. Unaendeleaje na katika kutafuta Maisha ya mafanikio? Leo nimekuletea mada nyingine ya muhimu sana baada ya mada ya mada ya mtaji. Haya mambo mazuri tunayozungumza hapa njia nzuri ya kupata matokeo ni kufanyia kazi haya unayojifunza bila kukata tamaa. Haijalishi utakutana na changamoto kiasi gani unatakiwa uendelee kupambana uzivuke ili ufikie mafanikio.

Mimi kazi yangu kubwa ni kuhakikisha wewe unapata mbinu bora za kushinda changamoto mbalimbali unazokutana nazo. Pamoja na kukupa njia mbalimbali za kufanya Maisha yako yawe bora.

Karibu sana kwenye mada ya leo ya kuanza biashara chini kabisa. (Starting from Zero/Scratch). Mara nyingi wengi wetu wanapenda waanze biashara leo na ianze kuwaletea mafanikio leo. Mtu anataka aanze biashara leo na aone faida kubwa baada ya muda mchache. Ukweli ni kwamba unapoanza biashara yeyote lazima ukubali kuwa mvumilivu sana. Ukubali kufanya hata kama upati matokeo muda huo huo. Kuna wakati biashara itajiendesha kwa hasara lakini pia unavumilia.
Unatakiwa ukubali kujifunza sana.

u Start Small (Anza na Kidogo)
Hapa kwenye kuanza na kidogo inategemea na aina ya biashara unayoifanya. Ila kwa kawaida kutokana na biashara nyingi kuwa na changamoto nyingi zinapoanza unashauriwa uanze na kidogo ili ujifunze kwanza. Kama huna mtaji (Tumeshazungumza mtaji sio Pesa tu) kama wengi wanavyolalamika ndio njia rahisi ya wewe kuanza na kidogo. Ndio njia rahisi ya wewe kujifunza mambo mengi na kukuza biashara kidogo kidogo.

u Start with what you have. (Anza na Ulicho Nacho)
Kuna tofauti ya kuanza kidogo na kuanza na ulichonacho. Kuanza kidogo ni kuanzia chini. Kuanza na ulichonacho ni kutazama una nini na unawezaje kutumia ulichonacho kuanza biashara. Mfano kama una simu ya mkononi ambayo inatumia mitandao ya kijamii unaweza kuanza kuonyesha wazo lako au bidhaa zako. Unaweza pia kuanza kukusanya oda ya bidhaa ulizonazo au hata kama huna.

Kuna siku nilimpatia mtu ushauri yeye alikua ana ujuzi juu ya dawa za asili yaani mitishamba. Tatizo lake lilikua ni mtaji alisema hana. Nikamwambia huna watu unaowajua wanaofanya kama wewe? Watu hao hawawezi kukuazima bidhaa au kukuuzia? Akaniambia anao! Nikamshauri hata kama hana mtaji pesa ana mtaji maarifa juu ya dawa za asili. Aanze kuwapa watu ushauri wakihitaji bidhaa badala ya kuwaelekeza kwa wenzake aende akazichukue auze abaki na faida. Faida akikusanya baada ya muda anaweza kujikuta anaweza kuendesha na kumiliki bidhaa zake mwenyewe.
Inawezekana hata wewe una vitu vingi sana vimekuzunguka lakini hujajua unawezaje kuvitumia kama mtaji na kuanzia navyo biashara.

SOMA: JINSI YA KUPATA MTAJI NA KUANZA BIASHARA

u Use Social Networks. (Tumia Mitandao ya Kijamii Kukuza Biashara yako)

Katika zama hizi za taarifa kitu ambacho huwezi kukiepuka kwenye biashara yako ni mitandao ya kijamii. Mitandao hii ina mchango mkubwa sana katika kukuza biashara yako na kuwafikia watu wengi Zaidi. Ukiweza kujua namna ya kuitumia mitandao hii utaweza kujenga biashara kubwa sana ambayo ina mafanikio.

Mitandao hii ni Facebook, Twitter, Instagram na WhatsApp. Hii ni baadhi tu ya mitandao unayoweza kuanza nayo katika kuifanya biashara yako kujulikana na kufikia wateja zaidi. Mitandao hii ina watumiaji wengi ambao unaweza kuwafanya marafiki na baadae kuwafanya kuwa wateja wako. Zipo mbinu mbalimbali za kuitumia mitandao hii ili kukuza jina jina lako au jina la biashara yako.

Njia ya kwanza ni kufungua kurasa zinazotambulisha biashara yako. Katika kurasa hizi unaweza kuanza kuwapa watu vitu vizuri ulivyonavyo. Watu wakiona unavitu vizuri watakufuata na kufanya biashara na wewe. Lakini hii inatokea pale wanapopata uhakika na uaminifu wako juu yao. Mimi binafsi nimefanya mauzo mengi sana ya bidhaa zangu kwenye mitandao ya kijamii pamoja na Blog kwa watu wengi ambao hata sijawahi kukutana nao kabisa. Hivyo ni uvumilivu na kutokata tamaa kunahitajika hapa.

Unahitaji kuwa na blog kwa ajili ya kuweka taarifa za kile unachokifanya. Tumia mitandao hii ya kijamii kuwaelekeza watu kwenye blog yako. Watu wakitembelea watajipatia zile huduma unazotoa.

Tuishie Hapa Leo tutaendelea na Mada nyingine wiki ijayo.
Kupata Ushauri Zaidi Bonyeza Hapa.

Kujiunga na Inuka Uangaze Bonyeza Hapa.

Kupata Vitabu Vya Sauti Sauti Bonyeza Hapa.

Kutengenezewa Blog Kwa Ajili ya Biashara yako Bonyeza Hapa
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com 
Blogs: www.jacobmushi.com,   www.jacobmushi.com 
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading