Jinsi ya kufikia Mafanikio

jacobmushi
2 Min Read
Goal setting( Weka Malengo),
Kua na malengo na hakikisha kila siku unafanyia kazi malengo yako. Malengo haya yalenge: Roho yako, Uchumi, Familia, Mahusiano, Kujiendeleza binafsi.

 Discipline( Kua na Nidhamu),
Nidhamu hii ni ya kujijengea na kuhakikisha kila siku unafanya yale yanayoleta manufaa kwako na kwa wengine. Watu wengu hua wanashindwa kusonga mbele zaidi na wanabaki pale pale kwa kukosa nidhamu. Mafanikio hayaletwi na ndoto kubwa au malengo makubwa au fikra chanya pekee yanaletwa na nidhamu. Umesema utaamka kila siku asubuhi saa kumi na moja je unafanya? Umesema utasoma kitabu kimoja kwa wiki unasoma? Umesema utapunguza kutumia mitandao ya kijamij vibaya unafanya?
Lazima uanze kua mkweli kwako mwenyewe lazima ufikie Mafanikio.

Persistence (Usugu Fanya mambo bila kuchoka Rudia rudia),

Kua sugu je changamoto unazozipitia zinakukatisha tamaa? Lazima ukubali kuumia ili upate vitu vizuri kupitia changamoto ni kuzuri sana kunakusaidia wewe uweze kubeba changamoto kubwa zaidi. Vumilia hadi uine mwanga. Kipindi hiki ndio jichanganye na watu ambao watakupa hamasa na sio kukukatisha tamaa.

 Focus(Fanya Jambo hadi upate matokeo),
Kitu kingine hua tunakosea ni kukosa focus.  Mtu anakimbilia kila fursa anayokutana nayo huwezi kupata matokeo makubwa na nguvu nyingi utakua umepoteza.
Fanya jambo moja na hakikisha limekutoa kwenye hatua moja hadi nyingine.
Kama ni biashara angalau mwaka upite na uwe umefanya kwa nidhamu na usugu ndipo usipoona mabadiliko unaweza kuacha.

 Time management( Pangilia Muda wako),
Kua mtu wa ratiba. Ratiba ya siku , week, mwezi, sana sana jitahidi uwe na ratiba ya week na siku. Hii itakuwezesha ujue ni nini unafanya huwezi kufanya kila jambo. Na hii itakuwezesha kila siku ujue unafanya nn ili ndoto na malengo yako yatimie.
Pangilia siku yako inayofuata kabla hujalala.
Pangilia week yako jumapili jioni.

Socialize with good people(Jichanganye na watu wazuri),
Jichanganye na watu ambao wanaongeza thamani kwenye maisha yako hii itakupa nafasi ya wewe kutimiza ndoto zako.

 Networking(Jenga mtandao wa watu wanaoweza kukusaidia kwa namna mbalimbali ikiwemo kununua bidhaa yako au huduma unayotoa, au hata kukutia moyo na wewe kufikia zile ndoto zako kubwa.
Asanteni sana.
Ukiweza kufuata haya utaweza kufikia ndoto zako na Mafanikio kwenye chochote unachokifanya..

Jacob Mushi
+255654726668

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading