Tabia ya kufanya jambo kidogo kisha ukaona hakuna matokeo na ukakata tamaa na kwenda kukimbilia kufanya jambo jingine inaweza kuwa sababu ya wewe kutokutimiza chochote kwenye Maisha yako. Kama huna uwezo wa kufanya jambo moja hadi ukahakikisha limekuletea matokeo anza mapema kuitengeneza.

Zipo sababu nyingi unaweza kuwa nazo za kwanini umeishia njiani lakini ukweli sababu hizo haziwezi kuwa suluhisho. Ukweli ambao wengi hawataki kuusema ni kwamba wengi wanakimbia changamoto na sio sababu zile wanazozisema kwa watu.

Chagua Mambo Madogo Madogo.

Ukitaka kujijengea tabia ya kukamilisha jambo, anza kufanya mambo madogo madogo na uhakikishe umeyamaliza. Kwa kupitia haya madogo utaweza kujitengenezea mtazamo wa ushindi ndani yako na utakusaidia kukamilisha yale makubwa na magumu.

Mfano kama wewe ni mwandishi na unataka kuandika kitabu lakini unashindwa jipe zoezi la kuandika maneno elfu moja kwanza kabla hujafikia kwenye kitabu. Tafuta mada mbalimbali ambazo utaziandikia hayo maneno hadi uone unaweza kuandika maneno elfu moja.

Usisikilize Kelele.

Jambo la msingi sana ni kutokusikiliza kelele za watu. Unapofanya kitu ambacho hujawahi kukifanya watatokea watu wengi sana ambao wanataka kukushauri namna ya kufanya. Watatokea watu ambao watatamani uje ufanye nao mambo Fulani.

Usikubali kabisa kuhamisha nguvu zako sehemu ambayo umeziweka na kuipeleka sehemu nyingine mpya. Kama umeamua unafanya jambo hakikisha umemaliza kwanza. Unapogawanya nguvu utashindwa kutimiza lile jambo moja unalofanya.

Kaa na Watu Wanaofanya Jambo Kama Lako.

Ulipokuwa shuleni kulikuwa na makundi ya kusoma, kama wewe unasomea masomo ya sayansi huwezi kuchagua makundi ya watu wanaosoma masomo ya Sanaa. Ni muhimu ukajua wewe ni kundi gani hivyo uchague watu ambao mtaweza kupeana mbinu mbalimbali za kuwasaidia kumaliza kazi.

Kama wewe unajichanganya na kila mtu unapokwama utakosa mtu sahihi wa kukusaidia. Wewe ni mfanyabiashara mdogo ukisema unajichanganya na waajiriwa unatakuwa unapotea.

Sijasema usiwe na watu ambao ni waajiriwa bali muda wako mwingi usiweke na watu ambao hawafanyi kile unachokifanya. Kuna kuambukizana tabia na mawazo kadiri unavyokaa na watu wasio kundi lako utajikuta unatamani kufanana nao.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Simu: 0654 726 668,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page  

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading