Jinsi ya kupata wazo la biashara:

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Habari za leo ni matumaini yangu kua unaendelea vyema kabisa. Leo tunakwenda kutazama njia tano za kupata wazo la biashara popote pale ulipo. Karibu ujifunze nami.
Zipo njia tano ambazo unaweza kuzitumia kubuni wazo bora la biashara katika jamii uliyopo nayo ni:
       1. Kwa kuangalia baadae(future): Kwa kuangalia jamii unayoishi unaweza kugundua baadae mabadiliko yatakuaje na wewe uweze kubuni wazo la biashara. Wapo waliogundua vitu ambavyo hadi sasa vinawaingizia pesa mfano aliegundua computer wakati anagundua computer zilikua zinahitahitajika tano tu duniani lakini sasa hivi kila mtu duniani anahitaji computer. Mwanzilishi wa mtandao wa facebook aliuanzisha kwa ajili ya wanachuo wenzake lakini sasa dunia nzima inautumia mtandao huu.
        2. Kwa kuangalia mazingira:  Kwa kuangalia mazingira unayoishi unaweza kugundua wazo la biashara itakayokuletea pesa nyingi sana angalia ni nini kinahitajika  kila kilete kwenye jamii yako wakpatie pesa. Kitu gani kimekosekana katika mazingira uliyopo anza na hicho utaweza kupata wazo bora la biashara.
       3. Kwa kusafiri: Unaweza kusafiri kwenda sehemu nyingine tofauti na uliopo na ukagundua vitu vingi sana ambavyo havipo kwenu ukarudi na kuvianzisha watu wakakupatia pesa.
       4. Kwa kupitia changamoto: Changamoto unazopitia leo zinaweza kua wazo la biashara. Umeenda hospitali ya maeneo unayoishi ukakuta wanatoa huduma mbovu na hawajali wagonjwa unaweza kuja na wazo la kuanzisha hospitali yako itayokua inajali wagonjwa na kutoa huduma bora. Changamoto yeyote ile unayoipitia wewe unaweza kubuni wazo la biashara kaa chini andika changamoto zote unazopitia na uone jinsi unavyoweza kuzibadili kua wazo la biashara.
       5. Kwa kuangalia asili: ni kitu gani cha asili kipo kwenu unaweza kukifanya kiwe pesa mfano wapo waliogundua nguo za kimasai, viatu, vinyago, na wanaziuza na wanatengeneza pesa. Anagalia asili ya kwenu kuna nini unachoweza kukibadili kiwe wazo la biashara.
Kumbuka: “ Usikubali kua wa kawaida kwani utapata matokeo ya kawaida, kua mbunifu kua tofauti na wengine” – Jacob Mushi

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading