JINSI YA KUZISHINDA CHANGAMOTO UNAZOKUTANA NAZO KWENYE UJASIRIAMALI NA BIASHARA.

jacobmushi
6 Min Read

Habari za leo Mwanamafanikio mwenzangu. Najua una pilikapilika nyingi kipindi hiki cha siku kuu. Lakini mimi pia bado nipo kwa ajili yako. Hivi unajua kwamba kipindi hiki watu ndio wananunua Zaidi? Kama ni hivyo basi wauzaji wananufaika sana. Je wewe umefanikiwa Kuuza chochote siku kuu hizi? Kama hujafanikiwa basi mwaka 2017 usikupite hivi hivi jipange tu ni kitu gani ungependa watu wanunue kutoka kwako vipindi vyote vya siku kuu.

Karibu kwenye Makala yetu ya leo tunazungumzia ni namna gani unaweza kushinda changamoto unazopitia kwenye ujasiriamali na biashara. Ni mambo ya muhimu sana ukiweza kuyafanyia kazi yote utafanikiwa. Usiogope changamoto kwani ndio zinatufanya tupande viwango. Matatizo au changamoto unazoziogopa leo na kuziruka zitakuja kukukwamisha huko mbeleni. Yaani kama sasa hivi ulitakiwa ujifunze kitu Fulani ukazembea ipo siku utatakiwa kutumia kile ulichotakiwa kujifunza na kwa kuwa uliruka basi utahitaji gharama kubwa Zaidi au ukose fursa iliyopo mbele yako.

  •  Never Give Up (Usikate Tamaa)

Kama umeamua kabisa kwamba utafanya hadi ufikie ndoto na maono yako usikubali kukata tamaa pale unapopitia changamoto. Jitie nguvu ili uweze kusonga mbele. Tafuta au namna ya kutatua tatizo sio kulikimbia. Safari ya mafanikio ni sawa na ile safari ya wana wa Israel kwenda Kaanani. Ukisema ukate tamaa urudi utarudi peke yako wenzako tunasonga mbele. Na ukisema ubaki hapo ulipo hutaweza kuishi kwani ni jangwani hivyo kuna siku utakosa maji na chakula na utakufa. Hivyo pia na mafanikioa usikubali kurudi nyuma wala kubaki hapo ulipo. Songa mbele

  • Never Stop Learning (Usiache Kujifunza)

Kamwe usiache kujifunza kuna njia nyingi za kujifunza sana. Kipindi hiki teknolojia imekua kubwa namna ya kupata taarifa mbalimbali za kukusaidia kwenye kile unachokifanya imekuwa ni rahisi sana. Kusoma vitabu imekua rahisi sana. Unaweza kuingia kwenye mtandao wa YouTube kwa kupitia simu yako au computer na ukajifunza mambo mengi mno kupitia videos. Unaweza kujifunza vitu mbalimbali kwa waliofanikiwa kwa njia rahisi. Hata kupitia group za WhatsApp kama upo kwenye kundi ambalo hujifunzi chochote hakuna haja ya kukaa humo maana ni kupoteza muda na pesa. Tafuta sehemu ambayo utajifunza hata kama utalipia pesa lakini uweze kusonga mbele kwenye kile unachokifanya.

  • Don’t Afraid to Fail (USIOGOPE KUSHINDWA)

Kamwe usiogope kushindwa ipo mifano mingi ya watu walionza vitu vyao lakini wakafanya na wakashindwa. Lakini kwao haikuwa ni mwisho walijaribu tena na tena hadi wakapata matokeo. Kama umeanza biashara kwa mara ya kwanza na ukapata hasara furahi sana maana umepata kitu cha kujifunza. Kama bado hujapata hasara yeyote au changamoto ogopa sana na angalia vizuri unachofanya kwani inawezekana husogei mbele umesimama sehemu moja tu. Ukianguka Inuka anza tena. Mtoto mdogo anapojifunza kutembea akianguka sio mwisho wa kutembea. Wewe ulipokuwa shuleni ukifeli jaribio sio mwisho wa kusoma tena. Hata ukifeli mitihani ya kumaliza shule nafasi za kurudia hua zipo. Hivyo hata katika biashara yako kushindwa kusikunyime nafasi ya kufanya tena.

  • Focus on Your Goals (Lenga kwenye Malengo yako)

Hakikisha unachokifanya kinalenga malengo yako. Yapo mambo mengi sana huku duniani ambayo ukiyasikiliza yanaweza kukutoa katika kile unachokifanya hivyo kujikuta hujafanya chochote. Huku duniani kuna fursa nyingi sana zinajitokeza kila siku kama utashindwa kulenga kwenye maono na ndoto zako utajikuta unapoteza mwelekeo na kufanya kila kinachokuja mbele yako. Jifunze kusema Hapana ukiwa umemaanisha hapana na Ndio ukiwa umemaanisha Ndio. Sio kila vita ni ya kwako sio kila pambano unatakiwa kupigana. Jiulize kwanza linaleta matokeo gani kwenye baadae yangu?

  • Find a Coach (Tafuta Kocha)

Tafuta Kocha au mtu wa kukushauri kwenye changamoto unazopitia. Mtu huyu unaweza kumpata kwa gharama ya malipo au bure kutokana na unavyofahamiana nae. Ila ukweli ni kwamba ushauri wa bure wengi hatufanyii kazi nimeshashauri watu wengi lakini huwa wanaondoka tu bila kufanyia kazi wanachoshauriwa. Wengine ukiwaambia ukweli huwa wanaondoka kimya na meseji hawajibu tena. Ukiwa na Kocha ambaye unamlipa na anakushauri lazima utatendea haki pesa yako. Lazima utafanyia kazi ushauri wake. Hakuna namna nyingine ya kufikia mafanikio bila kulipa gharama.

  •  Jichanganye na Wenye Mafanikio Zaidi yako Kwenye Kile unachokifanya.

Hakikisha umezungukwa na watu wengi wanaofanya vizuri kile unachokifanya kwani kwa kupitia watu hao utaweza kujifunza mambo mengi sana kwao. Utaweza kuwashirikisha changamoto zako na ukashauriwa. Inawezekana unachopitia alishapitia mtu Fulani na akaweza kuvuka hivyo ukapata msaada.

  • Tembelea Blog Hii Kila siku

Sio utani namaanisha kweli utembelee blog hii kila siku ili uweze kujifunza mambo mbalimbali ya kukuvusha kwenye changamoto uanzopitia. Kama umeona kuna mambo umeweza kuyapata ndani ya Blog hii yakakusaidia endelea kujifunza kila siku na kadiri tunavyoendelea kuwa pamoja utapata vitu vingi Zaidi na bora kwa ajili yako.

  • Jiunge na Programu Za Mafunzo

Kama unataka kuwa pamoja na mimi karibu Zaidi uweze kujifunza mambo mengi Zaidi na wanamafanikio wenzako jiunge na mtandao wetu wa Inuka Uangaze kwani utaweza kupiga Hatua mbalimbali katika Maisha yako ya mafanikio. Nipo kwa ajili ya kuhakikisha unafanikiwa kwenye kile unachokifanya wewe pekee ndiye unatakiwa uwe tayari.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author | Trainer | Entrepreneur

Simu: 0654 726 668 |0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading