Habari za leo Rafiki Yangu. Ningependa kukushukuru kwa wewe kuchukua muda wako na kusoma Makala mbalimbali ninazotuma kwenye email yako karibia kila juma.

Leo nina zawadi nzuri kwa ajili yako uliyoisubiria sana kwa muda mrefu. Kitabu Siri 7 za Kuwa Hai Leo tayari unaweza kukipata popote ulipo Africa Mashariki.

Watu wengi wanajiuliza kwanini Siri 7 Za Kuwa Hai Leo? Kwanza napenda kuwajibu kwa kuwauliza Swali moja Ni nani ajuae Kesho yake? Ni nani ajuae Siku ataondoka hapa duniani? Kwa jibu rahisi ni hakuna mwenye majibu. Hivyo kama hakuna mwenye majibu kila mmoja anatakiwa ajue ni namna gani anatakiwa kuishi Leo ili endapo itatokea kesho umeondoka hapa duniani uwe kuna kitu umeacha kama alama.
Ukweli watu wengi wamepoteza maana ya Maisha wengi wanafikiri Maisha ni kuwa na mwenzi mzuri, kujenga nyumba nzuri, kuzaa watoto na kuishi Maisha mazuri. Maisha ni Zaidi yah apo rafiki yangu. Unaweza kutimiza Lengo la kuoa mke au kuolewa na mume mzuri sana lakini ukafariki wewe kabla hata hujafurahia kumpata. Unaweza kutimiza lengo la kujenga nyumba nzuri sana na ya kisasa lakini ukafariki kabla hujaishi humo. Swali linakuja ni kitu gani kitaendelea baada ya wewe kuondoka duniani?
Umeacha mke/mume mzuri sana ataolewa/kuoa na mwingine. Umeacha nyumba nzuri watakuja kugawana ndugu zako au uliowaachia urithi. Je dunia itafaidika nini kwa uwepo wako hapa duniani? Hapo utakuta hakuna itakachofaidi.
Sasa nataka unielewe vizuri sijasema usioe au kuolewa, sijasema usijenge nyumba nzuri sijasema usiweke lengo la kuwa na gari au watoto. Maana yangu hapa ni hayo yasiwe malengo makuu ya Maisha yako. Kwanini yasiwe malengo makuu? Kwasababu unaweza kufa kabla hujapata vile ulivyoweka kama lengo kuu.
Lengo kuu la Maisha yako liwe ni kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Ukianza kujua hilo na ukalifanyia kazi utaondoka duniani ukiwa umeacha mabadiliko makubwa.
Hata kama tayari umeshapata vitu vyote ambavyo wengi huwa wanatamani kuwa navyo bado unaweza kuanza upya kulitimiza lengo kuu la Maisha yako.
Kwa kupitia kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo utaweza kugundua nini lengo kuu la Maisha yako hapa duniani. Utagundua kwamba Uliumbwa kwa kusudi lipi hasa na ufanyeje ili kufikia mafanikio kupitia hilo.
Kwasababu hakuna mwenye majibu ni siku gani ataondoka dunianu au kesho yake itakwenda kuwaje kupitia hiki kitabu utaweza kuishi leo vizuri sana. Na ukiweza kuishi leo vizuri Maisha yako yatakuwa na furaha na utaweza kutimiza kusudi.
Kupata kitabu Hiki wasiliana nami kwa Namba 0654726668 popote ulipo utatumiwa  bei ya kitabu ni Ths elfu kumi (10,000/=) gharama ya kutumiwa kitabu ni kuanzia Ths elfu tatu hadi elfu tano inategemea na sehemu uliyopo.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur
Phone: +255 654 726 668
Email: jacob@jacobmushi.com 
Blogs: www.jacobmushi.comwww.jacobmushi.com  
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading