“I have looked in the mirror every morning and asked myself: ‘If today were the last day of my
life, would I want to do what I am about to do today?’ And whenever the answer has been ‘No’ for
too many days in a row, I know I need to change something.” – Steve Jobs Apple
co-founder and CEO
Kama ukiambiwa leo ndio siku yako ya mwisho kuishi duniani utaendelea kufanya hicho unachokifanya sasa hivi?
Kama utaendelea kufanya ni wakati wako sasa uongeze bidii zaidi. Kama utaacha na kwenda kufanya kitu kingine. Hicho kingine ndio unatakiwa ukakifanye sasa hivi na hadi mwisho wa maisha yako.
Watu wengi tumekua tunafanya vitu bila vitu vyenyewe kutoka ndani ya mioyo yetu. Tunafanya vitu ambavyo sio makusudi ya sisi kuzaliwa duniani. Kama tutaweza kugundua kwa nini tunafanya hivyo tunavyofanya itakua na maana zaidi kuliko kufanya tu.
Kama hicho unachokifanya unafanya ili tu uingize pesa upo kwenye tatizo. Unachokifanya kinatakiwa kiongeze thamani kwenye maisha ya watu wengine. Kifanye maisha ya wengine yabadilike. Kama hakibadilishi maisha ya wengine ni tatizo.
Jiulize umekua mwalimu ili nini? Kwa sababu ajira zinapatikana kirahisi au ili uwasaidie wanafunzi wapate elimu?
Umekua askari ili nini? Ajira zilikua nje nje au ni ili wananchi wawe salama?
Kaa chini leo Jiulize hicho unachokifanya ni kitu gani kinakusukuma wewe ufanye?
Jiulize tena hili swali leo
“Kama Mungu akisema anataka kuwaondoa watu wote duniani ambao hawana kitu wanachofanya unafikiri ni kwa nini Mungu atakuacha wewe? “
Nakutakia wakati mwema wa kujiuliza maswali hayo kwenye hicho unachokifanya.
Karibu sana
Jacob Mushi
Phone 0654726668
Jipatie vitabu hapa… http://mushijacob.blogspot.com/p/vitabu-vya-sauti?m=1