Juhudi Zitaleta Matokeo.

Kama hutakata tamaa ipo siku matunda ya unachokifanya sasa yatakuja kuonekana.
Haijalishi hali uliyonayo sasa endelea kuongeza juhudi, hata kama huna anaekutia moyo au kukupongeza.
Ipo siku utayafurahia matunda ya kazi yako.

Hakuna jasho linalondoka bure. Usikubali kuachwa wala kurudi nyuma. Najua kuna nyakati ngumu zinafika hadi unajiuliza kama unafanya kitu sahihi kweli?  Mbona Matokeo huoni! 
Hakuna hata anaeona unachokifanya! 

Hiyo yote ni kipindi tu,  kitapita na utaanza kuona matunda.

Nimekumbuka kipindi cha nyuma wakati tunaotesha mahindi kuna nyakati jua lilikua linawaka mpaka unahisi haya mahindi yatakauka. Mahindi yananyauka kabisa kila mmoja anasema mwaka huu tumekosa.
Lakini kitu cha ajabu wakati tumeshakata tamaa kabisa tunawaza kung’oa mahindi yale tumpe ng’ombe, ghafla mvua zinaanza kunyesha.  Mahindi yanapata uhai upya na yaanza kukua kwa kasi, na baada ya muda tunafurahia mavuno.

Usikate tamaa kipindi jua linapokua kali,  unapohisi kunyauka. Mvua ipo njiani. Ukiona joto limezidi tambua kuna mvua kubwa sana itanyesha hivyo andaa mifereji ya kupitishia maji.

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Success Kingdom
Phone: 0654726668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com

This entry was posted in USIISHIE NJIANI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *