Habari za leo mwanamafanikio. Leo ninataka kukuonyesha mambo machache ambayo yanaonyesha wewe ni Mjasiriamali. Katika dunia ya sasa tunahitaji watu wengi ambao ni wajasiriamali watu ambao wako tayari kuchukua hatua kubadilisha Maisha ya wengine pamoja na ya kwao wenyewe.
1.Decision maker (Mfanya Maamuzi)
Kama wewe una uwezo wa kufanya maamuzi linapotokea jambo mbele yako bila kusita una sifa ya Mjasiriamali. Unapokutana na fursa Fulani nzuri unaweza kuitazama na kuamua moja kwa moja bila kutegemea ushauri wa watu wengine. Nimekuja kugundua kwamba tuna watu wengi sana wanaoshindwa kufanya maamuzi hadi wasikie wenzao wanasemaje. Kama wewe bado una tabia hii una safari ndefu sana ya kufikia mafanikio yako. Kama unakutana na fursa halafu ili ukubali hadi ukamuulize mwenzako mimi nakuhurumia. Na hii inatokana na uvivu wa kusoma na kutokuzijua taarifa za vitu mbalimbali. Hivyi unapokutana na kitu kipya unakuwa na mashaka ya kuamua. Mjasiriamali ana uwezo wa kutoa maamuzi na siku zote anakua na majibu matatu la kwanza ni NDIO, HAPANA, NALIFANYIA UTAFITI NITAKUJIBU BAADA YA MUDA FULANI. Kama wewe huwezi kuwa na majibu hayo na ukayasimamia huna sifa ya mjasirimali. Wengi wetu tukisema ndio hatumaanishi ndio tunasema ndio ili kumridhisha anaetuelezea wazo.
2.Risk taker (Asiogopa Hatari)
Mjasiriamali ni yule asiyeogopa hatari yeye wakati mwingine yupo tayari kuweka mtaji wake kwenye biashara ambayo hajawahi kuifanya lakini anaamini itamfikisha kwenye maono yake. Yupo tayari kwenda sehemu ambayo hajawahi kufika ili akaanzishe biashara mpya huko. Yupo tayari kuvumilia misukosuko yote anayoipata kipindi biashara inapoyumba au anapopata hasara. Yupo tayari kurudia biashara aliyofanya akashindwa.
Wewe umejaribu hatari ipi mpaka sasa ili tukuite Mjasiriamali? Umejaribu njia gani ya kufikia ndoto zako? Kama bado basi wewe sio Mjasiriamali. Kama unaogopa kupoteza pesa yako kidogo kwenye biashara ambayo hujawahi kuifanya au ni ngeni basi wewe huna sifa hiyo ya Mjasiriamali. Anza sasa kufanya na kujiingiza kwenye vitu ambavyo hujawahi kujaribu.
SOMA: USIYOYAJUA KUHUSU PESA HAYA HAPA
3. Self-confidence (Anaejiamini)
Mjasiriamali anajiamini kwa kile anachokifanya. Ana uwezo wa kuelezea vyema bidhaa yake bila kuogopa. Anajua anachokifanya na anapokwenda hivyo hana wasiwasi wa kushindwa au pale anapokosea. Jijengee sifa hii ya kujiamini na wewe utakaribia kuwa Mjasiriamali.
4. Leader (KIONGOZI)
Mjasiriamali yeyote ana sifa ya kiongozi kwasababu ameweza kujiongoza mwenyewe na anakwenda kuongoza biashara zake mwenyewe. Kama huna sifa ya kiongozi lazima utapoteza biashara zako pamoja na watu uliowaajiri. Kama huna sifa ya uongozi huwezi kufikisha maono yako mbali itakubidi uje uweke watu wenye maono makubwa Zaidi yako. Uongozi unaanza kwa kuweza kujiongoza mwenyewe.
5. Problem Solver (Mtatua Matatizo)
Ni mtu anaetatua matatizo ya watu popote anapokwenda huangalia watu wanapitia shida gani, ndipo huwaletea suluhisho na kutengeneza kipato. Kama wewe huwezi kuyaona matatizo ya watu kwenye jamii ni ngumu sana kuleta suluhisho. Hakikisha kila unapokwenda unatazama kwa jicho la tatu. Angalia ni kwa namna gani unaweza kuwasaidia wengine na wewe utengeneze kipato.
Matatizo yapo kila kona ndio maana watu hua wanashinda wakilalamika. Watu wenye sifa hii ya ujasiriamali huona tatizo haraka na kuleta suluhisho.
6. Vision (Mwenye Maono)
Ni mtu mwenye maono. Anaona mbali sana. Sio mtu anaefanya biashara ilia pate faida ya leo pekee. Lazima awe na maono ya kufikisha mbali wazo lake ili kuacha alama kwenye jamii inayomzunguka. Je wewe una maono? Unajua kuandika maono yako? Umeshaanza kuishi maono yako? Unachokifanya leo kinagusa nini kwenye maono yako?
Tunahitaji wajasiriamali wengi sana ili kuweza kutatua matatizo mengi yanayolikumba bara la Afrika. Unaweza kuwa mmoja wao.
Jacob Mushi,
Asante kwa maelezo nakubiliana na wewe hakika huo ndio ujasiriamali halisi, Asante kwa makala zako zinatutoa kiza Mungu akubariki sana.
Karibu sana Mkuu