KIBURI CHA MAFANIKIO

Habari za leo Rafiki, natumaini waendelea vyema na safari hii ya mafanikio. Ni muhimu sana kutokukata tamaa kwani huko mbele tuendako yako mazuri mengi sana. Njia zitaendelea kufunguka kuliko ulivyowahi kufikiri.

Leo twende tuangalie Kiburi cha Mafanikio. Hii ni hali au tabia ya mtu kuanza kujiona ameshapata kila kitu anachokitaka hivyo kuanza kufanya mambo yasiyofaa. 
Kiburi cha mafanikio ndio kimekuwa kinawaangusha wengi na kuwafanya wapoteze umaarufu,  mali zao,  vyeo na kadhalika.  Kiburi cha mafanikio kinaanza kuonekana sana pale mtu anapokua na vitu vya thamani vinavyoonekana na watu au anapopata watu wengi wanaomfuatilia.
Dalili za Kiburi cha Mafanikio.
Kutokujifunza tena, mtu mwenye kiburi cha mafanikio huacha kabisa kujifunza na kuona kwamba amefika.  Hajifunzi kwa wengine,  hasomi vitabu. Ukiona una dalili hizi ujue umeshapata kiburi cha mafanikio.
Kuwadharau wengine,  unakuta mtu ameweza kununua gari.  Basi watu wakajua si wengine wataanza na kumpigia simu aisee! Hapo ndio utajua mtu halisi yukoje na tabia zake. Wengine hata simu za ndugu zao wa karibu hawapokei tena. Marafiki zao wale waliokuwa wakitafuta pamoja hapokei simu zao tena. Kisa amepanda viwango. 
Starehe kwa wingi na kumsahau Mungu.  Wengi hapa ndipo wanapoanza kupotezea kila kitu.  Umeshapata pesa sasa unavaa vizuri na gari unalo. Na inawezekana pia nyumba ushajenga.  Basi wewe ni starehe kubadilisha wanawake wa kila aina au wanaume. Na ukumbuke ukiwa na pesa utakuwa na marafiki wengi wa kila aina. Unamsahau Mungu unakataa maonyo, na mwisho wako unakuwa mbaya zaidi.
Kumbuka usilewe mafanikio unapofanya vitu vya ajabu pale unapopata mali unaonyesha namna ulivyo na akili changa. 
Hutakumbukwa kwa mali ulizojikusanyia, utakumbukwa kwa vile ulivyowapa watu. 
Kama bado upo kwenye safari usikubali hata siku moja kuharibiwa na kiburi cha mafanikio.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author 
Success Kingdom
Phone: +255654726668 /+255755192418
Blog: www.jacobmushi.com
Email: jacob@jacobmushi.com
jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading