Mwisho wa kila tunachokipigania hapa duniani ni kifo, watu wengi wanafikiri kuna siku itafika sasa aanze kupumzika na kufurahia maisha ukweli ni kwamba usipofurahia maisha sasa hivi utajikuta muda umeshakwenda na vitu ambavyo ulitakiwa ufanye wakati fulani muda wake umepita.

Tunaambiwa kila jambo na wakati wake wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna, chochote unachokipanda sasa unatakiwa ujue kua utavuna, usitegemee matokeo ya haraka kama unafanya kitu sahihi,kwenye hii dunia hakuna jambo jema Zaidi ya kufanya yale yaliyo sahihi na kufurahi wakati tunaishi. Fanya kila jambo kwa wakati wake kuna wakati wa kuoa/kuolewa na uoe/uolewe usifikiri kwamba kuna wakati maalumu ambao utafika ndio mambo yatokee yenyewe uwezo wa kufanya wote Mungu amekupa wewe.
Bahati mbaya sana ni kwamba watu hawagundui kama wanapoteza muda hadi muda uwe umeshapotea, kuna mambo ambayo  ulitakiwa uyafanye ukiwa na miaka 25 hutaweza kuyafanya tena ukiwa na miaka 40, kama ni kufurahia ujana hujafurahia huwezi kufanya hivyo ukiwa na miaka 40, na hapa sizungumzii mambo maovu nazungumzia mambo yaliyo mema.

Hakuna ajuae siku yake ya kufa hivyo basi kama utafanya kila jambo kwa wakati wake hata ukiambiwa unaondoka leo bado kuna mambo utayafurahia maana tayari umeyafanya kwa wakati wake. Nikikutana na mtu akaniambia ameridhika na maisha aliyonayo hua namuuliza, Upo tayari kufa? Yaani ukiambiwa unaondoka leo duniani utakubali bila kuwaza vitu ambavyo hujavikamilisha? Kama umeridhika maana yake ni kwamba hautafuti kingine tena upo tayari kwenda.

Kitu cha muhimu cha kufanya kwenyemaisha
Fanya kile unachokipenda kwa bidii na kwa uwezo wako wote haijalishi una umri gani kama kinawezekana kufanyika muda huo kifanye, Furahia wakati unakifanya haijalishi kimefikia wapi furahia hii itakupa hamasa ya kuendelea kukifanya. Fanya mpaka upate matokeo unayoyataka haijalishi umefanya muda gani endelea kufanya.

Haijilishi muda umeshakupita kuna mambo umekosea hukuyafanya kwa wakati acha kujuta huwezi kubadili tena cha kufanya hapo ni kufurahia kile unachotakiwa ukifanye kwa wakati huo uliopo. Fanya mpaka uone moyo wake unasema kwa nilipofikia naweza kusema nimemaliza safari.

©Jacob Mushi 2016

2 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading