401; Kila Kitu Kilianza Kama Wazo.

jacobmushi
2 Min Read

Tangu mwanzo wa kuumbwa kwa ulimwegu huu kila kitu kilianza kama wazo. Mungu alikaa akawaza kuleta uhai katika sayari ya dunia baada ya sayari hii kuwa imejaa maji pekee yake.

Na tufanye mtu kwa mfano wetukwa sura yetu” (Mwanzo 1:26).

Na hakuishia hapo vitu vingine vyote ambavyo unaviona havikutokea tu vyenyewe bali vilitokana na mawazo yake mwenyewe.

Kitu ambacho sisi na Mungu tunatofautiana katika kufanya vitu ni kwamba yeye alikuwa anatamka halafu vitu vinatokea lakini sisi tunawaza, tunatamka halafu tunatenda ndio vitu vinatokea.

Ili lile wazo bora ambalo unalo liweze kutokea unatakiwa uanze kuliweka kwenye vitendo hadi litokee kwenye uhalisia.

Nasikiliza video ya mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple hapa yeye anasema alipokuwa mdogo karibu vitu vingi ambavyo vimetengenezwa kwenye Bidhaa za Apple aligundua kwa kufikiri sana. Hakupoteza muda kuangalia watu walishafanya vitu gani bali aliangalia akili yake inamletea mawazo ya aina gani.

Hata wewe inawezekana lile wazo ambalo unalo sasa hivi likaleta mapinduzi hapa duniani endapo tu utaanza kulifanyia kazi kwa bidii na nguvu kubwa. Mwanzilishi huyu anasema yeye alikuwa na uwezo wa kutengeneza compoter moja ndani ya siku 3 yeye mwenyewe. Hii inaonesha kwamba inatupasa tuweke bidii sana ndio itawezesha mawazo yetu yaje kuwa kweli.

Lazima ukubali kwamba bila vitendo hakuna kinachotokea. Kuwepo hapa duniani hiyo ni baraka kubwa sana ambayo Mungu ameshakupatia. Kuwa na uwezo wa kufikiri ni baraka kubwa sana ambayo Mungu amekuumba nayo.

Kilichobakia sasa ni wewe uanze kutumia zile baraka zilizopo ndani yako. Chukua hatua sasa vitendo ndio vitayaleta mawazo yako kwenye uhalisia. Usikubali watu wanaokataa mawazo yako wawe sababu ya wewe kuacha kile kilichopo ndani yako.

 

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
2 Comments

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading