Kile unachokipanda utavuna.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Ni mara nyingi  tumekuwa tunasikia usemi huu “kile apandacho mtu ndicho atakacho kivuna” ukweli ni huo lakini wengi hatuuchukulii usemi huu kwa makini. Wengi wetu tumekua tunapanda vitu vibays ndani ya akili zetu kila siku bila kujijua na wengine tunajua.

Unategemea ubongo wako uzalishe nini kama unaujaza Breaking News  za kila aina?  Unategemea ubongo wako ukupe matokeo gani kama wewe Tv, Magazeti, Habari za udaku ndio chakula cha ubongo wako?  Utakuletea kile unacholisha kila siku. Maisha yako hayatakaa yasogee maana unailisha akili ya vitu visivyo na afya. Akili haiwezi kuleta mawazo mapya kama imejaa Habari za ajali,  matukio ya ajabu ajabu tu kila siku. Hukupewa akili kwa ajili hiyo.

Ukitaka kua na akili inayozalisha Mawazo yatakayobadilisha jamii na maisha yako kwa ujumla kaa mbali na Tv Magazeti habari zisizokujenga,  watu hasi,  na kila aina ya uchafu ambao unaweza kuingia kwenye akili yako.

Unakuta mtu anakesha akiangalia movies za vita kila siku utafikiri tunakaribia kuingia vitani, mtu huyo sio mwanajeshi wala askari unaijaza akili yako vitu gani? Halafu Unategemea ikuletee matokeo ya aina gani?

Jijengee tabia ya kusoma vitabu na kufuatilia vitu vinavyoweza kukujenga,  vitu vitakavyobadili ufahamu wako ili uwe kua mzalishaji kwenye jamii yako.

Kile unacholisha ubongo wako ndio utakuja kukivuna huko mbeleni. Na siku zote mavuno yanakuwaga mengi kuliko mbegu zilizopandwa. Tegemea kupokea maradufu ya kile unachoweka kwenye akili yako kila siku.

Ukiweza kubadili namna unavyofikiri utabadili maisha ya namna unavyofikiri utaibadili kwa kubadilisha unavyoviweka kwenye akili yako.
Soma vitabu  chukua Hatua  Maisha yako yatabadilika.

©Jacob Mushi 2016
Mawasiliano  0654726668 E-mail jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading