Kitabu hiki nimeandika kwa ajili yako. Kuna mambo mengi sana ya kujifunza ndani ya kitabu hiki na nina imani kitakua ni sababu ya wewe kusogea katika eneo lile ulilokua na kwenda mbele Zaidi.

Utajifunza, Jinsi ya Kujua Kusudi Lako, Siri na Sababu za Kuwepo Hapa Duniani, Kugusa maisha ya wengine, Kufikia Ukuu, Kufika kilele cha Mafanikio, Kuishi maisha bora, Kutengeneza Na Mungu Wako, Kutambua kile Mungu ameweka ndani yako, Kufikia Ushindi Mkubwa.


Watu wengi wanaishi Maisha ambayo hayana mwelekeo, wanafanya kazi wasizozipenda, wanaishi Maisha wasiyoyataka kwa maana kuwa hayawapi furaha. Hii yote inaletwa na kutokujua sababu hasa ya wao kuwepo hapa duniani. Kitabu hiki kitakwenda kukufungua macho.

Utajifunza:

Ili uweze kuishi Maisha yenye mwelekeo mzuri na kujua ni kipi hasa unapaswa kufanya kila siku ni hadi utakapoweza kutambua kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Kitabu hiki kimeeleza namna yaw ewe kugundua kusudi lako.

Kila unachokifanya hapa duniani kinaongezeka sana endapo kitakuwa kinagusa Maisha ya wengine. Kiwango cha Maisha uliyogusa ndio kiwango cha mafanikio yako.

Ni alama gani unataka kuacha hapa duniani? Haijalishi umeshafanya makosa mangapi kuwepo kwako leo kunakupa nafasi ya kutengeneza historia mpya. Kitabu hiki kitakupa mwongozo huo.

Unatakiwa uishi Maisha ya ushindi kila siku kwenye kila unalolifanya. Utajifunza mbinu za kupata ushindi kwenye kila unachokigusa na mikono yako.

HAYA NI BAADHI YA MAONI MACHACHE NILIYOPATA KUTOKA KWA WATU AMBAO WAMESOMA KITABU HIKI.

“Kuwa Hai ni Zaidi ya kuwepo duniani, watu wengi sana wapo duniani lakini hawapo Hai, na wanaishi maisha ambayo si yao, Jacob Mushi kupitia Siri 7 za Kuwa Hai Leo ametengua kitendawili hicho, kwa kufichua mambo ya msingi ambayo ya kuishi maisha ya utoshelevu.”

Street Pastor,

Masanja Mkandamizaji

“Yaani ukianza kukisoma hutamani kuacha kwa jinsi kimebeba ‘facts’ Watu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa kumbe yamo kwenye “SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO.”  Ushauri wangu kwa Watanzania na wengine wanaoelewa kiswahili usikose nakala yako ya kitabu hiki kwenye library yako nyumbani. Thamani yake ni zaidi ya Tsh 10,000= utakayoitoa kukinunua. Hakika kitabadilisha maisha yako kuwa bora zaidi.”

Regula Tarimo

Mjasiriamali.

“Siri 7 za kuwa Hai Leo, ni kitabu kinachotoa muongozo wa kuishi maisha ya kulitimiza kusudi lako kwa mafanikio na furaha, Jacob Mushi amewasilisha kwa lugha inayoeleweka siri saba zitakazokufanya ujitambue na uanze kuwa hai. Kwa mtu yeyote mwenye kutaka kuishi maisha ya ushindi leo na kuacha historia nzuri napendekeza asome kitabu hichi.” 

Daudi Mwakalinga

Mkurugenzi/CEO wa kilimo.net.

“Kitabu cha Siri 7 Za Kuwa Hai Leo ni kitabu ambacho kila mtanzania hapaswi kukosa kukisoma. Nimekisoma na nimeona nguvu iliyoko ndani ya kitabu hiki pia nimeshuhudia watu wengi wakitoa sifa tele za kuweza kubadili maisha yao kupitia kitabu hiki. Napenda kusema kitabu hiki ni kama lulu kwa kila mtanzania kuweza kujifunza na kubadili fikra na maisha yake. “

Lazaro Samwel

Kocha wa Maisha, Mwandishi na Mjasiriamali.

Mtunzi na Mwandishi wa Kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.

Email; lazarosamweli41@gmail.com

“Huwezi kusoma kitabu hiki kisha ukabaki kama ulivyo. Uwe unafanya kazi au hufanyi kazi uwe mfanyabiashara,  mjasiriamali au mwimbaji kama mimi, ukisoma Siri 7 za kuwa hai leo, ni lazima utaongezeka kwenda hatua nyingne.“

Atosha Kissava

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania

Kinapatikana kwa mfumo wa softcopy kwa bei ya Tsh 10,000/= (elfu kumi). Lipia kwenda namba Tigopesa 0654 726 668 jina lilatokea Jacob Moshi. Ukishafanya malipo ya Kitabu tuma jina la kitabu pamoja na email yako na utatumiwa kwenye email yako mara moja.

Karibu Sana Rafiki.

Jacob Mushi,

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading