Habri rafiki, ni furaha yangu kuona bado unaendelea kufuatilia mtandao huu ili kujifunza. Nikupongeze kwa bidi yako hii katika kujifunza ipo siku itakuletea matunda. Ni kama mbegu unazopanda shambani lazima uzipe muda ndipo zitaanza kuchanua.
Huwezi kupanda miti wa mwembe kisha ukaweka mategemeo kama ya mtu aliepanda mahindi. Wewe wa mwembe itakuchukua muda mrefu sana hadi ufikie mavuno ya ulichokipanda. Aliepanda mhindi anatumia gharama ndogo, anasubiri muda mchache. Wewe uliepanda mwembe itakuchukua miaka kadhaa hadi uone matunda ya mwembe. Sasa watu hawajui ulichokipanda wataanza kukwambia “tulisema hayo mambo unayofanya hayana mafanikio.” “Ona wenzako tayari wameshaanza kuwa na Maisha mazuri.”
Usikate tamaa, unajua yule aliepanda mwindi mwakani itambidi arudi tena shamba kupanda. Wewe unaesubiria matunda ya mwembe, hautahitaji kupanda tena mwembe. Kazi yako itakuwa ni kunyeshea tu tena kidogo sana. Huku ukiendelea kufurahia matunda ya mwembe kila mwaka, au kila msimu wa maembe.
Maisha nayo yako hivyo, kile unachokifanya gharama kubwa unazolipa usitegemee matokeo ndani ya siku moja. Watu wanaweza tamani uwe kama mtu mwenye matumaini ya kupanda shamba la mahindi. Ulichokipanda ndio kinaamua na muda wa kusubiri.
Kwanini Usome Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO? Kitabu hiki nilitumia nguvu kubwa sana kukiandaa kwa ajili yako wewe ambaye umekuwa na changamoto ya kutokutambua kusudi la wewe kuwepo duniani. Pia nimeandika kwa ajili yakow ewe ambaye unaishi bila ya kujua kwanini unaishi kuna watu wengi wapo duniani lakini wapo kama wanapoteza muda au wanaosubiria siku ya kuondoka. Badala ya kuishi Maisha ya kukata tamaa unapaswa kujua ni namna gani unaweza kuishi Maisha yenye maana na utimilifu.
Watu wengi wamekuwa hawajui ni namna gani wanaweza kutumia zawadi ambazo Mungu ameweka ndani yao. Kitabu hiki kinakwenda kuwa sababu ya wewe kujua ni kitu gani Mungu ameweka ndani yako na ukitumie badala ya kuishi tu kama watu wengine.
Kila mmoja amekuja duniani kwa kusudi lake. Mtu mmoja alisema “Mungu ametupa vipaji na vipawa mbalimbali kama zawadi. Zawadi pekee tunayoweza kumrudishia ni kuvitumia vile vitu alivyoweka ndani yetu.” Wakati sahihi wa kutumia vitu hivyo ni sasa, ni Leo. Mahali sahihi kwa kutumia vitu hivyo ni hapa duniani. Kitabu hiki kinakwenda kuwa msaada mkubwa kwako ili uweze kurudisha zawadi ambazo Mungu ameweka ndani yako kwa kuziishi.
HAYA NI BAADHI YA MAONI MACHACHE NILIYOPATA KUTOKA KWA WATU AMBAO WAMESOMA KITABU HIKI.
“Kuwa Hai ni Zaidi ya kuwepo duniani, watu wengi sana wapo duniani lakini hawapo Hai, na wanaishi maisha ambayo si yao, Jacob Mushi kupitia Siri 7 za Kuwa Hai Leo ametengua kitendawili hicho, kwa kufichua mambo ya msingi ambayo ya kuishi maisha ya utoshelevu.”
Street Pastor,
Masanja Mkandamizaji
“Yaani ukianza kukisoma hutamani kuacha kwa jinsi kimebeba ‘facts’ Watu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa kumbe yamo kwenye “SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO.” Ushauri wangu kwa Watanzania na wengine wanaoelewa kiswahili usikose nakala yako ya kitabu hiki kwenye library yako nyumbani. Thamani yake ni zaidi ya Tsh 10,000= utakayoitoa kukinunua. Hakika kitabadilisha maisha yako kuwa bora zaidi.”
Regula Tarimo
Mjasiriamali.
“Siri 7 za kuwa Hai Leo, ni kitabu kinachotoa muongozo wa kuishi maisha ya kulitimiza kusudi lako kwa mafanikio na furaha, Jacob Mushi amewasilisha kwa lugha inayoeleweka siri saba zitakazokufanya ujitambue na uanze kuwa hai. Kwa mtu yeyote mwenye kutaka kuishi maisha ya ushindi leo na kuacha historia nzuri napendekeza asome kitabu hichi.”
Daudi Mwakalinga
Mkurugenzi/CEO wa kilimo.net.
“Kitabu cha Siri 7 Za Kuwa Hai Leo ni kitabu ambacho kila mtanzania hapaswi kukosa kukisoma. Nimekisoma na nimeona nguvu iliyoko ndani ya kitabu hiki pia nimeshuhudia watu wengi wakitoa sifa tele za kuweza kubadili maisha yao kupitia kitabu hiki. Napenda kusema kitabu hiki ni kama lulu kwa kila mtanzania kuweza kujifunza na kubadili fikra na maisha yake. “
Lazaro Samwel
Kocha wa Maisha, Mwandishi na Mjasiriamali.
Mtunzi na Mwandishi wa Kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.
Email; lazarosamweli41@gmail.com
“Huwezi kusoma kitabu hiki kisha ukabaki kama ulivyo. Uwe unafanya kazi au hufanyi kazi uwe mfanyabiashara, mjasiriamali au mwimbaji kama mimi, ukisoma Siri 7 za kuwa hai leo, ni lazima utaongezeka kwenda hatua nyingne.“
Atosha Kissava
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania
Kama bado ulikuwa hujasoma kitabu hiki ni mambo mengi sana umekuwa unayakosa hivyo chukua hatua sasa upate nakala yako.
Maisha ya wengi yamekuwa ya mateso, wengi hawajui wanapoelekea hawafanyi kazi ambazo zinawapa Amani ya moyo wanafanya kwasababu Maisha yanawabana. Wengine wanafanya vitu sio kwasababu ni vitu sahihi ila ni kwasababu wamewakuta watu wengine wanafanya huku duniani. Hakuna Maisha ya hovyo kama kuishi Maisha kwa kuangalia wengine wanafanya nini ndipo na wewe ufanye. Kwa kupitia kitabu hiki utaweza kupata jawabu la Maisha yako ni kitu gani hasa unapaswa kufanya kwenye dunia hii.
Napenda kukwambia usikubali kuishi Maisha ya kulazimishwa kama kuna kitu hukipendi kwenye Maisha yako sasa hivi kuwepo kwako hai ni nafasi ya kukibadilisha. Kama Maisha unayoishi hayakusababisha ujisikie Amani ya moyo na ujione unaelekea sehemu katika macho yako ya ndani ni wakati wako wa kusoma kitabu hiki.
Tumezaliwa duniani tuje tutawale lakini sio wote wanatawala. Wengine wanatawaliwa inawezekana wewe ni mmoja wao. Hukuzaliwa kuja kuishi Maisha ya aina hiyo. Umezaliwa ukiwa na kusudi maalumu kabisa la kuwepo hapa duniani. Usikubali kuishi Maisha ya kitumwa Maisha ambayo hujui unapoelekea unawafuata watu kila anaekuja mbele yako unatamani kwenda nae.
Kitabu hiki kinakufaa sana ili uweze kushi Maisha ya ushindi kila siku.
Unaweza kukipata kwa nakala ya softcopy yaani nakutumia kwenye email yako
Kitabu hiki bei yake ni Tsh 10,000/= elfu kumi tu.
Unaweza kufanya malipo kwenye namba TigoPesa 0654726668 au 0755192418 Mpesa majina ni Jacob Moshi yatakayotokea kwenye malipo.
Ukifanya hivyo nitumie ujumbe kwenye mojawapo ya namba hizo kisha unaniambia jina la kitabu na unataka utumie kwa email au kwa gari.
Karibu sana
Usiishie njiani