Kama Hujui unapokwenda usiwaambie watu wakufuate. Hii ni pamoja na mke yaani usitafute mke kwanza kama hujajua unapokwenda.

Mwanamke mwenye akili anafata maono yako,  sio pesa zako, sio umaarufu wako. Mwanamke anaekufuata kwasababu ya vitu vinavyoonekana kwa nje mara inakuaga ni tamaa
ila sio mara zote

“Marehemu Dr.  Munroe katika moja ya Mafundisho yake anasema Mwanamke swali la kwanza la kumuuliza mwanaume  Kabla hujauliza kama unapendwa Muulize anakwenda wapi”

Familia nyingi zinateseka huku duniani,  ndoa zinavunjika kwasababu ya wanaume waliokosa maono.

SOMA: NGUVU YA TAARIFA KATIKA MAONO NA NDOTO ZAKOl

Mambo ya Muhimu Kutambua.

? Wewe ni nani? (Kusudi)
Ni muhimu sana Kujitambua wewe ni nani hapa duniani,  upo kwa Kusudi gani hapa duniani. Hii itakuwezesha upate mwelekeo wa maisha yako

?Unakwenda wapi? (Maono)
Maono ndio yanakupa mwelekeo wa maisha. Kama huna maono basi hujui unapokwenda. Na kama hujui unapokwenda huwezi kwenda au Utakwenda popote.  Mwanaume ni lazima uwe na Maono.

Unahitaji nini cha kukuwezesha kufika huko uendako? (Maarifa/Ujuzi)

Hapa tunakuja kwenye upande wa Maarifa na Ujuzi. Ukishatambua kwamba wewe ni Daktari,  na unataka uje kuwa Daktari bingwa wa Magonjwa fulani lazima utatumia muda mwingi kujifunza zaidi juu ya hiyo fani yako.
Huwezi kutumia muda mwingi kujifunza siasa.

Unahitaji wakina nani? (Marafiki, Mke(Kama Hujaoa bado) ,)
Ukishatambua wewe ni nani, Unakwenda wapi na ukaanza safari yako. Utaanza kuvutia watu wa kufanana na wewe.  Hata marafiki zako watakuwa zwanaoendana na kule unapokwenda. Utaweza pia kujua ni mke wa namna gani anakufaa kama bado hujaoa.

Ukijua unapokwenda na ukaanza kuishi kwa namna inayofanania,  utaanza kuwavuta watu unaofanana nao na kuwasukumu wasio fanana na wewe.

Mara nyingi nimekuwa naona wanaume wanahimizwa kuwa na vitu vya muhimu kama,  Mahali pa kuishi yaani nyumba, na vitu vingine vya muhimu vya ndani. Vilevile Aweze kujilisha na aweze kuwalisha wengine. Hivi pia ni vitu vya muhimu sana lakini kama utakuwa navyo vyote ukamiliki maghorofa na kila kitu, halafu Hujui Kusudi la wewe kuwepo hapa duniani bado huwezi kuwa na ndoa au maisha yenye furaha.

Kwasababu gani sasa? Kwanza ni rahisi mno kukosea kuchagua mke kama hujui kusudi la wewe kuwepo hapa duniani.

 

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading