Home » KONA YA BIASHARA » KONA YA BIASHARA: Epuka Tabia Hii

KONA YA BIASHARA: Epuka Tabia Hii

Jambo Moja unalopaswa kukumbuka kila wakati unapokuwa kwenye biashara yako ni hili EPUKA MAZOEA. Mazoea ni sumu mbaya sana ambayo inaweza kukusababisha ukaanza kumtafuta aliekuloga kumbe chanzo ni mazoea.

Unapoanza biashara unakuwa na hamasa kubwa unawahudumia watu vizuri sana sasa shida inakuja pale unapokuwa tayari umeshasimama. Biashara inaenda vizuri umepata wateja wa kutosha na biashara ina mzunguko mzuri.

Hapo ndipo unapoanzia kujilogea, unasahau kabisa yale mambo ya msingi yaliyokuweka hapo ulipo. Unasahau huduma bora kwa wateja unawahudumia kwa mazoea. Huangalii tena ubora kwenye bidhaa zako. Kila kitu unakifanya hovyo.

Kuna msemo mmoja wa wahenga unasema “ukimsifia mgema tembo hulitia maji” mgema ni mtengenezaji wa pombe aina ya tembo. Sasa ukishaanza kumsifia ooh unatengeneza pombe tamu ataanza kuitia maji ili auze nyingi.

Sasa na wewe epuka tabia hizi za mazoea endelea kuweka ubora kila siku kwenye kila unachokifanya. Jiwekee misingi kwenye biashara yako na usikubali mtu yeyote awe mfanyakazi au yeyote aivunje.

Jua kwanini upo kwenye biashara usisahau hata siku moja tatizo unalotatua. Maana hilo ndio linakuweka sokoni.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

About

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

%d bloggers like this: