Pasipo maono kwenye biashara yeyote watu wengi huishia njiani. Kama hakuna unapotaka kufika utakuwa unaridhika na kile unachokipata kila siku. Kama huna maono huwezi kuwa na mipango mipya wala mabadiliko labda tu hali iwe mbaya. Biashara nyingi zilizokosa maono huendeshwa kiholela, wamiliki wa biashara na hata wafanyakazi hawajui ni wapi wanataka kwenda. Wengi wanaishia kuangalia tu faida wanayoipata kila siku basi.

Kama unaanza biashara yeyote leo ambayo unataka kudumu nayo muda mrefu Zaidi ya miaka kumi basi ni muhimu kuwa na maono. Tengeneza picha kubwa ambayo itakupa mwelekeo wa kila unachokifanya.

Kumekuwa na tabia ya watu kukimbilia kila fursa inayotokea mbele yao, hasa pale ambapo mambo yanapokuwa magumu kwenye biashara ambayo upo inakuwa ni rahisi sana kukimbilia kitu kingine kipya. Kama wewe una maono makubwa kwenye biashara yako, na maono hayo umeyafanya yakawa wewe. Yaani umeyaingiza kwenye akili yako kiasi kwamba kila unachokifanya kinahusiana na maono yako sio rahisi hata chembe ujikute unabebwa na fursa nyingine. Labda tu iwe inakufanya uweze kufikia maono yako.

Andika maono yako kwenye kitabu chako na uyatafakari mara kwa mara, asubuhi na jioni hadi picha hiyo ijengeke kwenye ufahamu wako. La sivyo itakuwa rahisi sana kuhamishwa na mafanikio ya wengine. Akitokea mtu ameanza biashara Fulani na ameweza kununua gari baada ya muda mfupi utajikuta unakata tamaa kwenye maono yako wewe.

mojawapo ya mazoezi magumu ni kuchagua washirika wa biashara, watu kwa mara ya kwanza wanaweza kuvutiwa sana na mawazo yako lakini sio kila anaevutiwa na kuhamasika anafaa. Maono yako yataamua na yatakupa msaada wa kujua ni aina gani ya watu wanafaa. Miongoni mwa marafiki zako wapo watakaokupinga na wapo ambao wataamua kwenda na wewe.

Bonyeza hapa Upate kItabu cha USIISHIE NJIANI, TIMIZA NDOTO YAKO.

Unapokosea kuchagua ujue umejibebesha mzigo wa matatizo kwenye safari yako ya mafanikio. Unaweza kuingia na mtu kwenye biashara yeye ana mategemeo ya kuona faida kwa haraka kumbe faida zitaanza kuonekana miaka ijayo mtu wa hivyo atakusumbua, au kukuacha njiani.

Kuna nyakati utapitia magumu mengi, utapata hasara, utatengwa na watu, utasemwa vibaya. Maono yako ndio yatakupa nguvu, ukiitazama ile picha kubwa unayoina baadae unapata nguvu Zaidi na kusonga mbele. Wengi wasio na matumaini hukimbia biashara zinapoyumba au kupata hasara.

Maono yako ndio yanatakiwa yawe chanzo kikuu cha kukutia moyo. Kuna nyakati utakuwa mwenyewe hadi watu wa karibu yako utaona kama hawakusemeshi, wengine watasema umechanganyikiwa. Lakini kama una tumaini ndani yako utaendelea kusonga mbele bila ya kukata tamaa.

Bonyeza hapa upate KITABU: Mafanikio Kwenye Biashara.

Ibrahimu baba wa Imani alipokuwa anazungumza na Mungu, Mungu alimwambia atazame juu angani. Kisha akamuuliza “Unaona Nini?” Ibrahimu akasema anaona nyota, akamwambia kama utaweza kuzihesabu huo ndio utakuwa uzao wako. Wakati huo anaambiwa hivyo bado hakuwa na mtoto yeyote na Sarah mke wake alikuwa tasa. Nguvu kubwa ya maono yako ipo kwenye kuona, kile unachokiona ndio kinakwenda kutokea. Bila kujali upo kwenye hali gani wakati huo unapoitengeneza picha yako.

Hii ni sehemu katika kitabu change kipya usikose nakala yako kitakapokuwa tayari. Usikose Kitabu changu kipya “MAFANIKIO KWENYE BIASHARA”

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading