Zipo Sababu nyingi za kushindwa kwa biashara mbalimbali lakini hizi ni mojawapo ya vyanzo vinavyofanya watu washindwe. Kama unataka kuwa na mafanikio tengeneza tabia njema ambazo zinawavutia wengi kuwa karibu na wewe. 

Kukasirika Hovyo Hasa Mteja Anapokuja na Malalamiko.

Kama unashindwa kuvumilia malalamiko ya wateja wako una hatari kubwa ya kuwapoteza wote. Jaribu kuwa msikivu haijalishi mteja anasumbua kiasi gani wewe kukasirika hakutasaidia. Jukumu lako ni kutatua matatizo ya wateja wako. Sehemu wanayopaswa kuleta malalamiko ni kwenye biashara yako na sio sehemu nyingine.

Kuwa mpole na uhudumie kwa tabasamu wakati wote. Ni sawa na daktarin kuona kelele za maumivu ya wagonjwa kama usumbufu huyo atakuwa hana wito wa udaktari. Ni sawa na muuguzi kuona kinyaa kwwenye vidonda vya mgonjwa wake. Itakuwa haina maana ya yeye kuwepo hapo hospitali.

Wahakikishie wateja wako kuwa wamefika mahali salama na matatizo yao yanakwenda kutatuliwa wafanye wafurahie kuwepo kwenye biashara yako. Hadi mtu ameamua kuja kufanya biashara na wewe lazima ameshakuwa na Imani na wewe. Usikubali kuiondoa Imani yake juu yako.

Kutoa Huduma Mbovu kwa Wateja Walioomba Wapunguziwe Bei.

Kama utashindwa kumhudumia mtu vizuri kwasababu tu ameomba apunguziwe bei unajiharibia mwenyewe. Kila jambo baya ufanyalo kwa mteja ujue ni tangazo umepeleka kwa wengine wasiokujua na wanaokujua. Ukiwafanyia vizuri na wao wanaanza kuwa wa kwanza kuelekeza wengine waje kwako. Usikubali kutoa huduma mbovu kwa vyovyote vile. Kama mtu ameomba apunguziwe na unaona bei yake itakufanya ufanye kazi mbovu ni bora ukaacha kabisa kufanya kazi yake.

Kuweka Kipaumbele kwenye Pesa Kuliko kwenye Huduma Bora.

Kama utakuwa unaangalia faida unayopata pekee badala ya kutazama unachotoa kama kinaendana na faida unayotaka utaanza kukimbiwa na wateja. Ukifikia mahali upo tayari umuuzie mtu kitu hata kama hakina thamani kubwa kwasababu ni mgeni ujue unaanza kutumbukia shimoni.

Pesa ni ya muhimu sana lakini inapopatikana bila ya thamani kutolewa inakuwa ni hatari kwa ukuaji wa biashara yako.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading